Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
12 Novemba 2020 11:39:54
Dalili za ugonjwa wa moyo
Magonjwa ya moyo ni moja ya magonjwa yanayoongezeka kwa kasi katika nchi zinazoendelea. Magonjwa haya yameshakuwepo kwa kipindi kirefu katika nchi zinazoendelea kutokana na mitindo ya maisha.
Magonjwa ya moyo yapo ya aina tofauti, yapo yale ya kurithiwa ambapo mtoto huzaliwa nayo, na pia yapo yale yanayotokana na maambukizi pamoja na magonjwa ambayo si ya kuambukiza.
Makala hii imejikita kuangalia dalili mbalimbali ambazo zinaweza kumaanisha kuwa mtu huyu ana tatizo la moyo. Kumbuka dalili za magonjwa ya moyo huweza kufanana na dalili za magonjwa mengine kama vile, magonjwa ya figo na ini.
Dalili za ugonjwa wa moyo kwa wanawake huwa tofauti na wanaume, mfano wanaume hupata sana maumivu ya kifua, wakati wanawake hupata dalili ya kifua kizito na kushindwa kupumua vema. Hii ndio maana dalili katika makala hii zimegawanywa kwa wanawake na wanaume na kutokana na visababishi pia halisi vya tatizo la moyo.
Dalili zisizotegemea jinsia na umri
Dalili kwa ujumla za ugonjwa wa moyo huwa ni
Maumivu ya kifua
Kubana kwa kifua
Kukandamizwa kwa kifua au kutohisi vema ndani ya kifua
Kuishiwa pumzi
Maumivu, udhaifu au kuhisi baridi kwenye miguu na mikono
Maumivu ya shingo, taya, koo na maeneo juu ya tumbo au nyuma ya mgongo
Dalili za ugonjwa wa moyo zinazosababishwa na mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Mapigo ya moyo kwenda kasi
Kutikisika kwa maeneo ya kifua karibu na moyo
Mapigo ya moyo kwenda taratibu
Kutohisi vema ndani ya kifua
Kizunguzungu
Kichwa kuwa chepesi
Kuzimia
Dalili za magonjwa ya moyo yanayosababishwa na madhaifu katika maumbile ya moyo
Kuwa na rangi ya bluu kwenye ngozi
Kuvimba kwa miguu
Kuvimba kwa tumbo
Kuvimba kwa maeneo yanayozunguka macho
Kuishiwa pumzi wakati wa kunyonya kwa vichanga
Kutoongezeka uzito vema kwa watoto vichanga
Kuchoka haraka wakati wa mazoezi
Kuishiwa pumzi kwenye shughuli ndogo tu
Kuvimba kwa kiwiko cha mguu, miguu na kanyagio
Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na udhaifu kwenye misuli ya moyo
Kupumua kwa shida wakati unataka kusimama au kutembea
Kuvimba kwa miguu, kiwiko cha mguu na kanyagio
Uchovu
Maopigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Kizunguzungu, hisia za kichwa chepesi na kuzimia
Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na maambukizi kwenye moyo
Homa
Kuishiwa pumzi
Kuvimba kwa miguu na tumbo
Kubadilika kwa mapigo ya moyo
Kikohozi kikavu
Harara kwenye ngozi
Dalili za ugonjwa wa moyo kutokana na magonjwa ya milango ya moyo
Uchovu
Kuishiwa pumzi
Mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Kuvimba kwa kiwiko cha mguu na miguu
Kuzimia
Dalili za magonjwa ya moyo kwa wanawake
Kutohisi vema ndani ya kifua
Maumivu ya kifua katikati ya kifua
Kuhisi kifua kama kimekandamizwa na kitu kizito
Maumivu au kutojihisi vema mkono wa kushoto na mabega
Kuishiwa pumzi bila kuw ana maumivu ya kifua
Kichefuchefu na kichwa kuwa chepesi
Kuzimia
Kutokwa kwa kijasho cha baridi
Dalili za ugonjwa wa moyo kwa wanaume
Maumivu ya kifua kama vile ya kuchana kitu
Kuhisi mgandamizo kwenye kifua
Kuhisi kifua kimejaa kw andani
Maumivu kwenye mkono wa kushoto, taya au nyuma ya mgongo
Kuishiwa pumzi
Kutokwa na kiijasho cha baridi
Kichefuchefu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:47
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Heart. Heart attack. https://www.heart.org/en/health-topics/heart-attack/warning-signs-of-a-heart-attack/heart-attack-symptoms-in-women. Imechukuliwa 12.11.2020
2.Medal news today. Signs of heart disease in men.https://www.medicalnewstoday.com/articles/322237. Imechukuliwa 12.11.2020
3.Symptoms of a heart attack. American Heart Association Go Red for Women. https://www.goredforwomen.org/en/about-heart-disease-in-women/signs-and-symptoms-in-women/symptoms-of-a-heart-attack. Imechukuliwa 12.11.2020
4.Pagidipati, N. Clinical features and diagnosis of coronary heart disease in women. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 12.11.2020
5.Heart attack symptoms. Office on Women's Health. https://www.womenshealth.gov/heart-disease-and-stroke/heart-disease/heart-attack-and-women/heart-attack-symptoms. Imechukuliwa 12.11.2020
6.Ischemic heart disease. National Heart, Lung, and Blood Institute. . https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/ischemic-heart-disease. Imechukuliwa 12.11.2020