top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

24 Machi 2020 09:32:13

Dalili za upungufu wa damu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Dalili za upungufu wa damu

Upungufu wa damu mwilini kwa jina la kitiba Anemia humaanisha upungufu wa seli nyekundu za damu zinazoitwa hemoglobin. Kiwango cha kawaida cha chembe za damu za haemoglobin kweney mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa Kila mililita ya damu, kiwango pungufu ya Hapo mtu mtu husemekana kuwa ana tatizo la upungufu wa damu.


Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) viwango vya himoglobin mwilini hutofautiana kati ya jinsia moja na nyingine, umbali kutoka usawa wa bahari, ujauzito, uvutaji wa sigara.


Hemoglobin hupatikana ndani ya chembe nyekundu za damu, kazi yake kuu ni kubeba na kusafirisha gesi ya oksijeni kutoka kwenye mapafu na kusambaza kwenye maeneo mbalimbali ya mwili.

Vijenzi vya Hemoglobin ni pamoja na madini chuma na protein ambazo vyanzo vyake ni chakula


Visababishi vya upungufu wa damu mwilini


Kisababishi kikuu vya kupungukiwa damu mwilini huwa ni kupata lishe duni haswa yenye upungufu wa madini chum ana vitamin B12 na A. visababishi hivi vinaweza kuwekwa kwenye makundi kama yalivyoorodheshwa hapa chini


Kupungua uzalishaji wa chembechembe za damu mwilini

Hii ni kutokana na lishe duni upungufu wa madini muhimu ya chuma, upungufu wa vitamini kama vitamina B12 na A


Kuongezeka kwa uharibifu wa chembe nyekundu za damu

Uharibifu huu unaweza kutokana na ugonjwa wa hemolitiki anemia ambalo huweza tokana na magonjwa ya kurithi kama ugonjwa wa seli mundu(siko seli), thalassemia. Madhaifu ya autoimuni, kuferi kwa urojo wa mifupa, madawa


Magonjwa ya kuambukizwa

Magonjwa kama malaria, TB, Virusi vya UKIMWI na maambukizi ya parasaiti wanaopelekea upunguwa wa damu unaofanana na ule wa kukosa madini chuma mfano kama Necator americanus na Ancylostoma duodenale, Trichuris trichiura, Schistosoma mansoni, Schistosoma haematobium na Schistosoma japonicum


Kupoteza damu nyingi

Kunaweza kutokea kutokana na ajali, kufanyiwa upasuaji, wakati wa kujifungua, magonjwa aina Fulani kama himophilia, leukemia, ugonjwa wa ini, menorajia, piriodi kali,, endometriosisi, thrombosaitopeni, ugonjwa wa von Willebrand, upungufu wa vitamin K. pia matumizi ya dawa aina Fulani mfano dawa za kuyeyusha damu(kama warfarin), dawa za antibayotiki zikitumika kwa muda mrefu, tiba mionzi, aspirini na dawa zingine jamii ya NSAIDs.


Dalili za upugufu wa damu mwilini/Ishara za Kupungua damu


Dalili za anemia hutegemea na kisababishi, dalili zilizoorodheshwa hapa chini ni dalili za ujumla na baadhi tu ambazo huonekana sana kwa wagonjwa.


  • Mapigo ya moyo kwenda kasi

  • Kuhisi mapigo ya moyo

  • Kupumua kwa shida

  • Kulegea kwa mwili

  • Maumivu ya kifua

  • Maumivu ya kichwa

  • Kuhisi kizunguzungu

  • Kupungua au kukosa umakini

  • Daimeshia

  • Weupe usio wa kawaida kwenye macho, mdomo, ulimi, viganja, kucha na hata ngozi

  • Kucha kua na umbo la kijiko ( koilonchia) na kukatika katika kirahisi

  • Dalili za moyo kuferi kama kuvimba miguu, kushindwa kupumua wakati wa kulala

  • Manjano

  • Mkojo kuwa na rangi ya brauni au nyekundu

  • Kwa Watoto kushindwa kukua vema]

  • Dalili za mawe kwenye kibofu cha nyongo

  • Kupata maambukizi kirahisi


Madhara ya upungufu wa damu


Madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wa damu ulio sugu ni pamoja na;


  • Kupata arizima

  • Uchofu mkali

  • Moyo kutanuka(kuwa mkubwa)

  • Kuferi kwa moyo

  • Kwa wanajawazito kujifungua kabla ya wakati

  • Kifo


Namna ya kujikinga na upungufu wa damu


Tumia vyakula vyenye madini chuma

Tumia vyakula vyenye madini chuma kama nyama ya ng’ombe na nyama aina nyingine, maharagwe, vyakula vya jamii ya kunde, mimea jamii kijani iliyokolea, na matunda yaliyokaushwa.


Vyakula vyenye madini ya folate

Hupatikana kwenye matunda na juisi ya matunda, mboga za majani za rangi ya kijani iliyokolea, mimea jamii ya kunde, maharagwe, karanga, na mimea mingi ya mbegu kama ngano, mchele n.k


Kutumia vyakula vyenye vitamin

Kama vyakula vya Vitamin B12 kwa wingi. Kama vile nyama, vyakula kutokana na maziwa ya Wanyama, mbegu zilizolowekwa, vyakula kutokana na soya. Vyakula vyenye vitamin C kwa wingi mfano matunda jamii ya machingwa na juisi yake, pilipili, broccoli, nyanya, matikiti maji, matunda ya stroberi. Vitamini C husaidia sana kwenye ufyonzaji wa madini chuma hivyo husaidia kuzuia upungufu wa damu.


Kumbuka

Soma zaidi makala za vyakula na vitamini katika tovuti hii, bonyeza kitufe katika menyu ya tovuti hapo juu ili kuchagua chakula na mazoezi au virutubisho A-Z kupata makala hizi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.WHO, Anaemia overview https://www.google.com/url?q=https://www.who.int/health-topics/anaemia&sa=U&ved=2ahUKEwjIssKAkrHoAhWnlXIEHbcqAIkQFjASegQIAhAB&usg=AOvVaw2A8X2xSIzXQLrEzlfBetAT . Imechukuliwa 23.3.2020

2.The American journal of clinical nutrition. Parasitism and Anemia by Z. FARID, M.D., D.T.M. & H. (ENG.) etal. https://academic.oup.com/ajcn/article-abstract/22/4/498/4733011?redirectedFrom=fulltext. Imechukuliwa 24.03.2020

3.National Heart, Lung and blood Institute, hemolytic anemia https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/hemolytic-anemia imechukuliwa 24.03.2020

4.WEBMD understanding anemia symptoms https://www.google.com/url?q=https://www.webmd.com/a-to-z-guides/understanding-anemia-symptoms&sa=U&ved=2ahUKEwjDkcPCnbHoAhXO-6QKHaVNAZwQFjAMegQICBAB&usg=AOvVaw310ie4aUqIX0su5MZooCcc .Imechukuliwa 23.3.2020

5.Healthline, what you need to know about hemorrhage. https://www.healthline.com/health/bleeding#causes imechukuliwa 24.03.2020

6.Mayo clinic. Anemia symptoms and causes. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/anemia/symptoms-causes/syc-20351360 imechukuliwa 24.03.2020

7.MEDICINENEWSTODAY. Everything you need to know about anemia. https://www.google.com/url?q=https://www.medicalnewstoday.com/articles/158800&sa=U&ved=2ahUKEwjIssKAkrHoAhWnlXIEHbcqAIkQFjARegQIARAB&usg=AOvVaw2DUevZof2H5E-eIqmfBXUp . Imechukuliwa 23.3.2020

8. Maswali na majibu kutoka kwa Wataalamu tiba wa ULY CLINIC

bottom of page