Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
20 Machi 2020, 16:46:44
Dalili za UTI kwa watu wazima
Mfumo wa mkojo umegawanyika katika sehemu kuu mbili, mfumo wa mkojo wa chini na mfumo wa mkojo wa juu, mfumo wa chini umetengenezwa na mrija wa urethra, kibofu cha mkojo na mirija miwili ya ureta.
Mfumo wa juu wa mkojo umeundwa na figo ambazo huchuja maji mwilini na kutengeneza mkojo.
Maambukizi mfumo wa juu ya mkojo hutokea endapo maambukizi ya mfumo wa chini wa mkojo yamesambaa na kwenda kwenye figo. Maambukizi kwenye figo huwa hatari sana kwani yanaweza kusababisha bakteria kuingia kwenye damu kwa kuwa damu nyingi hupita kwenye figo kwa ajili ya kuchujwa. Hata hivyo maambukizi ya mfumo wa juu wa mkojo huleta dalili kali na hutishia uhai wa mtu.
Kazi kubwa ya mfumo wa mkojo ni kuondoa sumu, uchafu na maji ya ziada mwilini
Ni vimelea gani husababisha uti?
Uti kwa asilimia zaidi ya 90 husababishwa na bakteria ainayeitwa ya escherichia coli ambaye hupatikana katika mfumo wa chakula. Bakteria wengine wanaoweza kusababisha uti ni pamoja na enterococcus faecalis, enterobacteriaceae na staphylococcus saprophyticus, na wakati mwingine uti inaweza kusababishwa na fangasi . Bakteria aina ya Staphylococcus Saprophyticus huleta maambukizi kwa wasichana wadogo na dalili zake huamka haraka sana.
Dalili za uti ya mfumo wa chini wa mkojo kwa wanawake na wanaume
Dalili anazopata mwanamke ni sawa na zile anazopata mwanaume ambazo ni ;
Maumivu wakati wa kukojoa
Maumivu ya tumbo haswa ya chini ya kitovu
Mkojo kutoa harufu kali pamoja na kubadilika rangi ya mkojo na kuwa kama mawingu
Hisia za maumivu ya kuungua na mkojo wakati wa kukojoa
Kukojoa mara kwa mara
Kushikwa na hamu ya kukojoa ila mkojo unatoka kidogo
Homa
Uchovu wa mwili
Kichefuchefu na kutapika
Dalili za maambukizi mfumo wa juu wa mkojo
Maumivu nyuma ya mgongo chini ya mbavu, pande mmoja au pande zote mbili
Maumivu ya kiuno
Kutokwa na damu wakati wa kukojoa
Homa kali
Kichefuchefu na kutapika
Kutetemeka mwili
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:04:25
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Wein aj, et al., eds. Infections of the urinary tract. In: campbell-walsh urology. 11th ed. Philadelphia, pa.: elsevier; 2016. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020
2. Ferri ff. Urinary tract infection. In: ferri's clinical advisor 2017. Philadelphia, pa.: elsevier; 2017. Https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 17.03.2020
3. Bladder infection (urinary tract infection—uti) in adults. National institute of diabetes and digestive and kidney diseases. Https://www.niddk.nih.gov/health- information/urologic-diseases/bladder-infection-uti-in-adults. Imechukuliwa 17.03.2020
4. Urinary tract infections (utis). The american college of obstetricians and gynecologists. Https://www.acog.org/patients/faqs/urinary-tract-infections-utis. Imechukuliwa 17.03.2020
5. [Guideline] Gupta K, Hooton TM, Naber KG, et al. International clinical practice guidelines for the treatment of acute uncomplicated cystitis and pyelonephritis in women: A 2010 update by the Infectious Diseases Society of America and the European Society for Microbiology and Infectious Diseases. Clin Infect Dis. 2011 Mar. 52(5):e103-20. [Medline]. [Full Text].
6. [Guideline] Wagenlehner FM, Schmiemann G, Hoyme U, Fünfstück R, Hummers-Pradier E, Kaase M, et al. [National S3 guideline on uncomplicated urinary tract infection: recommendations for treatment and management of uncomplicated community-acquired bacterial urinary tract infections in adult patients]. Urologe A. 2011 Feb. 50(2):153-69. [Medline]. [Full Text].