top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

Dkt. Adolf S, MD

8 Julai 2023 12:46:35

Haja ngumu baada ya kujifungua
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Haja ngumu baada ya kujifungua

Kupata haja kubwa ngumu ni tatizo linalotokea sana kwa wanawake baada ya kujifungua. Kubadili mtindo wa maisha, matumizi ya vyakula vyenye nyuzinyuzi na maji kwa wingi huzuia na kupunguza dalili.

 

Visababishi

Haja ngumu baada yakujifungua inadhaniwa na wanasayansi kusababishwa na uwepo wa kiwango kikubwa cha homoni progesterone wakati wa ujauzito sambamba na mabadiliko ya matumizi ya chakula.

 

Dalili za haja ngumu baada ya kujifungua

Kupata haja ngumu baada ya kujifungua huweza ambatana na dalili zingine kama vile:

  • Maumivu ya tumbo au kujihisi vibaya tumboni

  • Kutumia nguvu nyingi kusukuma kinyesi

  • Kuwa kinyesi kigumu kinachoshindwa kupita kwenye tundu

  • Hisia za kubakisha kinyesi baada ya kumaliza haja

  • Kutoa kinyesi kigumu chenye nundu (mithiri ya kinyesi cha mbuzi)

 

Sababu zinazoongeza hatari ya haja ngumu baada ya kujifungua

Hofu ya kwenda chooni kwa sababu ya kuwa na bawasili, kufanyiwa upasuaji wa kuongeza njia ya uzazi, upasuaji wa kujifungua ni vihatarishi vinavyopelekea kupata haja ngumu baada ya kujifungua.

 

Sababu zingine

Matumizi ya dawa zenye madini chuma kama dawa ya kuongeza damu na kuacha mazoezi baada ya kujifungua huwa kihatarishi kingine cha haja ngumu baada ya kujifungua.

  

Tiba ya haja ngumu

Kuelewa vema kuhusu kisababishi cha tatizo husaidia kuzuia na kutibu tatizo la haja ngumu baada ya kujifungua.

 

Haja ngumu hutokea endapo kinyesi kinakaa kwenye utumbo mpana kwa muda mrefu kuliko kawaida kupelekea kufyonzwa maji yake hivyo kufanya iwe ngumu, kavu na kutoka kwa shida.

 

Mabadiliko ya Maisha kwenye chakula na mazoezi hushauriwa wakati wa ujauzito kama kinga ya tatizo hili. Vyakula vinavyotakiwa ni vile vyenye nyuzinyuzi kwa wingi mfano matunda na mboga za majani na matumizi ya maji kwa wingi.

 

Mazoezi ya wastani yanayoongezeka kwa kiwango cha kustahimilika na salama kwa mjamzito hushauriwa kufanywa na mama aliyejifungua mara anapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo. 

 

Matumizi ya dawa ya kulainisha matumbo inaweza kuwa njia nyingine ya kuzuia na kutibu tatizo hili. Usalama wa matumizi yake kama kinga na tiba inatakiwa kuzingatia faida na madhara yake mwilini.

 

Tiba mbadala

Tiba ya acupuncture na dawa asilia zilizoonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu tatizo hili zinaweza kutumika pia. Inashauriwa kutumia dawa zilizofanyiwa tafiti na kusajiliwa kuwa salama kutumika kwa binadamu.

 

Makala hii pia imejibu maswali kuhusu

Kukosa haja kubwa baada ya kujifungua

 

Wapi unaweza kupata maelezo zaidi

Pata maelezo zaidi katika makala zifuatazo:

Konstipesheni

Kinyesi kama cha mbuzi

Dawa za kutibu konstipesheni

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Julai 2023 12:50:43

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Turawa EB, et al. Interventions for preventing postpartum constipation. Cochrane Database Syst Rev. 2020 Aug 5;8(8):CD011625. doi: 10.1002/14651858.CD011625.pub3. PMID: 32761813; PMCID: PMC8094226.

2. Cullen G, et al. Constipation and pregnancy. Best practice & research. Clinical Gastroenterology2007;21(5):807‐18.

3. Glazener CMA, et al. Postnatal maternal morbidity: extent causes, prevention and treatment. British Journal of Obstetrics and Gynaecology 1995;102:282‐7.

4. Zainur RZ, et al. Postpartum morbidity ‐ what we can do. Medical Journal Malaysia 2006;61:5.

5. Balch PA. Prescription for Nutritional Healing: a Practical A‐to‐Z Reference to Drug‐free Remedies using Vitamins, Minerals, Herbs & Food Supplements. 5th Edition. Penguin: New York, 2010.

6. Koltyn KF, et al. Psychological effects of an aerobic exercise session and a rest session following pregnancy. Journal of Sports Medicine and Physical Fitness 1997;37(4):287‐91.

7. Candy B, et al. Laxatives or methylnaltrexone for the management of constipation in palliative care patients. Cochrane Database of Systematic Reviews 2011, Issue 1. [DOI:10.1002/14651858.CD003448.pub3]

8. Jia G, et al. Treatment of functional constipation with the Yun‐chang capsule. Journal of Gastroenterology and Hepatology2009;25(3):487‐93.

bottom of page