top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

17 Aprili 2020 18:58:37

Homon Imbalance- dalili
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Homon Imbalance- dalili

Kuharibika (kupotea) kwa uwiano wa homoni mwilini ikijulikana na watu wengi na kitiba kama tatizo la 'Homon imbalance' au homoni imbalansi ni tatizo ambalo linaweza kutokewa kwa mtu yeyote awe mwanaume au mwanamke Watoto na watu wakubwa.


Kuna dalili nyingi zinaweza kutokea kumaanisha tatizo la homoni imbalance, dalili hutegemea aina ya homoni iliyoathiriwa.


Kuharibika kwa uwiano wa homoni mwilini hutoka na kupungua au kuongezeka kwa homoni kwenye damu. Mabadiliko yanaweza kuwa kidogo sana lakini bado yakaonyesha dalili za kuonekana.


Katika Makala hii imezungumzia kuhusu kutowiana kwa homoni mwilini kwa wanawake, wanaume, Watoto na wanawake walio kwenye komahedhi, visababishi na matibabu ya kutowiana kwa homoni.


Visababishi


  • Matibabu ya saratani(dawa za satatani)

  • Haipothairoidizimu

  • Haipathairoidizimu

  • Sindromu ya kushing

  • Ugonjwa wa Kisukari

  • Haipogonadizimu

  • Thairoidaitizi

  • Aina Fulani za dawa

  • Msongo wa mawazo

  • Kutokula vema

  • Magonjwa ya kula

  • Haipaplezia ya tezi ya adreno

  • Saratani mbalimbali kama saratani tezi ya pituitari na thairoidi

  • Uvimbe usio saratani kwenye tezi mbalimbali

  • Matumizi ya dawa za homoni


Visababishi kwa wanawake

  • Ujauzito

  • Kunyonyesha

  • Ugonjwa wa polisistiki ovari

  • Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango

  • Kutojitosheleza awali kwa ovari

  • Komahedhi kabla ya wakati

  • Komahedhi


Dalili


Dalili kwa Watoto

  • Kutoota vema kwa nywele

  • Sauti kutokuwa laini kwa wanawake, na kutokuwa nzito kwa wanaume

  • Kuchelewa kukua kwa uume na korodani

  • Kukua sana kwa misuli ya mikono na miguu kusikowiana na kiwiliwili

  • Kutokupata misuli kwa wanaume

  • Kuota kwa matiti makubwa kwa wanaume na wanawake kutokukua kwa matiti

  • Kutokupata hedhi kwa wakati

  • Kutokukua vema au kutokukua kwa wanawake na wanaume


Dalili kwa wanawake

  • Ngozi kufubaa kwenye maeneo ya mikunjo haswa shingoni na maeneo ya kinena na chini ya matiti

  • Maoteo ya vipele mshikizo

  • Kukauka kwa uke(uke kukosa majimaji)

  • Kusinyaa kwa uke

  • Maumivu wakati wa kujamiana

  • Kutokwa jasho wakati wa usiku

  • Kupata hedhi nzito au isiyoeleweka

  • Kuota nywele za wanaume mfano ndevu n.k

  • Kuota chunusi

  • Nywele kukatika kirahisi

  • Kuongezeka uzito au kushindwa kupunguza uzito


Dalili kwa wanaume

  • Kukua kwa matiti kama ya wanawake

  • Kupungua hamu ya kujamiana

  • Ugumba

  • Kupungua kwa ndevu au kutoota kwa ndevu na nywele zsehemu zingine

  • Mifupa kuvunjika kirahisi

  • Matatizo ya kutosimamisha uume

  • Kutokuwa makini

  • Maumivu ya matiti

  • Kupoteza ujazo wa misuli ya mwili/kutokupata misuli mikubwa.


Dalili za ujumla

Kumbuka dalii hizi hutegemea aina ya homoni yenye shida. Si lazima mtu awe na dalili zot endo asemekane kuwa ana tatizo la kutowiana kwa homoni mwilini.


  • Kuwa na uzito mkubwa usioelezeka au kupungua uzito usioelezeka

  • Jasho kupita kawaida

  • Kupata shida ya kulala

  • Kushindwa kuhisi joto au baridi

  • Kuwa na ngozi kavu sana

  • Kubadilika kwa shinikizo la damu

  • Kubadilika kwa mapigo ya moyo

  • Mifupa kuwa mikavu

  • Kubadilika kwa kiasi cha sukari kwenye damu

  • Woga na wasiwasi

  • Kuchoka kusiko kwa kawaida

  • Kuongeza kiu

  • Hali ya huzuni

  • Kichwa kuuma

  • Tumbo kujaa gesi

  • Hamu ya kula kubadilika

  • Kupunguza hisia za mapenzi

  • Kuwa na nywele nyembamba

  • Ugumba

  • Uso kujaa

  • Uso wa duara

  • Kutokuona vizuri

  • Shingo kuvimba

  • Maumivu ya matiti

  • Sauti kuwa nzito kwa wanaume


Visababishi


Sababu zinazopelekea homoni kutokuwiana ni kama :


  • Kuwa na msongo wa mawazo wa muda mrefu

  • Kisukari

  • Kuzalishwa kwa wingi kwa homoni ya glucagon

  • Kuzalishwa kwa wingi kwa Homoni ya Insulin

  • Kuzalishwa kwa homoni chache za tezi ya thyroid

  • Kuzalishwa kwa wingi kwa homoni za tezi ya thyroid

  • Wingi au uchache wa homoni ya parathyroid

  • Mlo dhaifu

  • Kuwa na uzito kupita kiasi

  • Dawa za mbadala za homoni

  • Kuwa na uvimbe kwenye pituitary

  • Kuzalishwa kwa wingi wa homoni ya Cortisol (Cushing’s syndrome)

  • Kuzalishwa kwa uchache kwa homoni ya aldosterone na cortisol (Addison’s disease)

  • Kupata mzio mkali

  • Saratani zinazohusisha mfumo wa homoni

  • Matibabu ya kikemikali na mionzi

  • Kuwa na iodine chache

  • Kuwa katika mazingira yenye sumu kama za kuulia wadudu na magugu


Matibabu ya nyumbani


  • Kuzuia hali zinazoamsha kutokwa na jasho- mfano hali ya hewa ya joto, vyakula vyenye viungo, na vinywaji vya moto.

  • Ondoa vinyweleo vya ziada kama kwa kutumia mashine ya kunyoa nywelkula vyema- kula mlo kamili. Jifunze Zaidi kuhusu mlo kamili sehemu nyingine katika tovuti hii.

  • Tumia vilainishi kuondoa kutojihisi vema ukeni kama vile Mafuta ya glycerini na yenye petroliamu.

  • Punguza uzito mkubwa. Unapopunguza uzito unaondoa matatizo mengi ya homoni imbalance kwa wanawake na wanaume. Soma Makala zingine katika tovuti hii ya namna ya kupunguza uzito au omba ushauri kutoka kwa madaktari wa ulyclinic.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:02:52

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.MedicalNewToday.Hormone.Imbalance.https://www.medicalnewstoday.com/articles/321486. Imechukuliwa 17/4/2020

2.HormoneHealth.HormoneImbalance.https://hormonehealth.co.uk/blog/10-warning-signs-you-may-have-a-hormonal-imbalance-and-what-to-do-about-it/. Imechukuliwa 17/4/2020

3.ParsleyHealth.HormoneImbalance.https://www.parsleyhealth.com/blog/hormonal-imbalance-symptoms/. Imechukuliwa 17/4/2020

4.Healthline. Hormonal imbalance home remedy. https://www.healthline.com/health/hormonal-imbalance#natural-remedies. Imechukuliwa 17.04.2020.

5.Davidson’s Essential of medicine Edited by Alastair Innes ISBN 9780702030000 Ukurasa wa 329

bottom of page