Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
8 Novemba 2021, 08:26:59
Jipu njia ya haja kubwa
Jipu kwenye njia njia ya haja kubwa ni mkusanyiko wa usaha sehemu ya kupitishia haja kubwa ama ndani ya kifuko kinachotunza kinyesi kabla hakijatoka au maeneo karibu na njia ya haja kubwa.
Visababishi
Nini husababisha majipu sehemu hizi?
​
Baadhi ya visababishi vingine vya maumivu ama miwasho sehemu za haja kubwa ni
​
Matatizo kwenye mfumo wa utumbo mpaka kama tatizo la vidonda vya Crohn’s
Miwasho mikali sana sehemu za siri- husababisha na mipasuko na endapo ikiambukizwa basi hutengeneza jipu
Saratani
Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI
Michaniko kutokana na maambukizi ya kirusi cha Herpes
Vidonda vya kaswende(ugonjwa wa zinaa)
Matumizi ya baadhi ya dawa kama nicorandil na predinisolone
Uchafu katika maeneo ya haja kubwa/kutokanana tabia ya kutojisafisha vema
​
Vihatarishi
Vihatarishi vya kupata jipu/usaha sehemu za siri
​
Kujamiiana kinyume na maumbile/ wanaume kwa wanaume au mwanaume kwa mwanamke
Mipasuko kwenye njia ya haja kubwa inayoweza kusabaishwa na haja ngumu
Kuziba kwa tezi za njia ya haja kubwa kutoka an amaambukizi au uchafu
Matumizi ya dawa za kutibu saratani
Kuwa na ugonjwa wa kisukari au divetikulaitizi
Magonjwa ya autoimyuni kama-ugonjwa wa crohns na asaletivu kolaitizi
Matumizi ya dawa jamii ya corticosteroid na zingine zinazoshusha kinga za mwili
Kudhoofika kwa kinga ya mwili kutokana na maambukizi kama VVU/UKIMWI
Dalili
Dalili ni kama vile;
​
Kuvimba maeneo yanayozunguka sehemu ya haja kubwa , na maumivu yasiyoisha ya kuchoma. Maumivu yanaweza kuwa makali wakati wa kupitisha haja kubwa
Kupata choo kigumu
Kutokwa usaha kwenye njia ya haja kubwa
Mwili kuchoka, homa, kutetemeka na jasho wakati wa usiku(haswa kwa majipu yaliyondani zaidi)
Rangi ya ngozi kwenye maeneo ya haja kubwa kubadilika kuwa nyekundu, kuwa ngumu maeneo ya uke (kwa watoto rangi huonekana kuwa nyekundu na hulia lia kutokana na maumivu ya jipu hilo
Dalili zingine zinaoweza kujitokeza kama madhara ya jipu hili ni;
​
Kupata shida wakati wa kuanza kukojoa
Maumivu wakati wa kukojoa
​​
Vipimo
​
Vipo vipimo vya ian tofauti unaweza kufanyiwaikitegemea hali yako na nini daktari ameona, vipimo hivi vitampa uwanja daktari wa kutambua madhara au matatizo mengine yanayoweza kuwa yamesababishwa na jipu hili. Wakati mwingine kipimo kinaweza kisihitajike kama daktari ameona tatizo lako halihitaji vipimo zaidi mbali na kipimo cha wali cha kuchunguza mwili kwa macho.
Baadhi ya vipimo ni
​
Kipimo cha ultrasound ya njia ya haja kubwa(mara chache kitahitajika)
Kipimo cha MRI au CT scan(mara chache kitahitajika)
Kipimo cha FBP(mara chache sana kitahitajika)
Vipimo vya magonjwa ya zinaa kama UKIMWI, kaswende, kisonono n.k
Kipimo cha kutambua ugonjwa wa crohn's
Kipimo cha kutambua saratani
​
Matibabu
​
Jipu sehemu za siri haliwezi kupona tu kwa matibabu ya kupambana na bakteria. Matibabu kwa ujumla huhusisha;
​
Dawa za kuua maambukizi ya bakteria( si kila dawa inasaidia)
Upasuji- hufanyika kwa kuondoa usaha na kisha kidonda huwa hakifungwi ili kuruhusu usaha utoke
Baada ya upasuaji utashauriwa kukalia maji yenye madawa ya kupambana na bakteria, maji ya uvuguvungu ili kufanikisha usaha kutoka na kupunguza maumivu
Dawa za maumivu pia hutolewa na mtu hushauriwa kutumia chakula laini
Baada ya upasuaji unaaweza kuruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyohiyo ama kusubiri kwa siku kadhaa.
Kwa kawaida utapona na kurejea kwa kwa hali yako ya akwaida ndani ya wiki 2 hadi 3
Kinga
​
Kuwa na tabia ya kujisafisha vema kwenye tundu la haja kubwa- Wakati wa kujisafisha hakikisha unapokuwa unajisafisha uwe unajaribu kama kutoa haja kubwa ili sehemu ya utumbo itokeze nje uisafishe vema.
​​
Kwa watoto wachanga, kubadilisha pampasi mara kwa mara baada ya mtoto kujisaidia na kumsafisha vema kutazuia kupata majibu sehemu hizi
​
Tumia kondomu wakati wa tendo la kujamiana endapo unajamiana kinyume na maumbile.
​
Acha kujamiana kinyume na maumbile
​​
Madhara
​
Kutokwa na usaha njia ya haja kubwa kunaweza kupelekea kupata fistula kati ya njia ya haja kubwa na njia ya mkojo. Kwa wanawwake wanaweza kupata fistula kati ya njia ya haja kubwa na uke. Fisstula hii husababisha kuingia kwa kinyesi kweney mkojo au kutokea ukeni
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Novemba 2021, 08:26:59
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada