Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
25 Julai 2023 17:58:36
Kubeua
Kubeua ni njia ya mwili kuondoa hewa iliyozidi kwenye mfumo wa juu wa umeng’enyaji wa chakula ambayo mara nyingi humezwa wakati wa kula au kunywa. Hewa hii kwa mara chache huweza kuingia tumboni lakini mara nyingi hujikusanya kwenye umio.
Visababishi vya kumeza hewa
Mtu anaweweza meza hewa ya ziada na kufanya abeue kwa kufanya mambo yafuatayo:
Kula kwa haraka
Kunywa kwa haraka
Kutafuna bablishi
Kumumusa pipi
Kuvuta sigara
Kuvuta kitu kingine
Kunywa vinywaji vilivyotiwa kaboni kama soda
Baadhi ya watu humeza hewa bila hata kuwa wanakula au kunywa kama njia ya kuepuka woga.
Vihatarishi
Baadhi ya vihatarishi vya kubeua ni kama vifuatavyo;
Kuwa na ugonjwa wa kucheua tindikali
Maambukizi ya Helicobacter pylori anayesababisha vidonda vya tumbo
Dalili zingine
Kubeua kunaweza kuambatana na dalili zingine kama vile
Kiungulia
Maumivu ya tumbo
Namna ya kupunguza kubeua
Kufanya mambo yafuatayo yanaweza kupunguza kumeza hewa na kubeua:
Kula au kunywa taratibu.
Kula taratibu kunaweza kufanya upunguza kiwango cha hewa unachomeza. Kuepuka kula wakati una haraka au msongo hupunguza kiwango cha hewa kinachoingia kwenye tumbo.
Epuka kunywa vinjwaji vilivyotiwa kaboni na bia
Vinywaji hivi huzalisha hewa ya ukaboni ambayo husababisha kubeua
Acha kutafuna bablishi au kumumunya pipi
Ulaji wa pipi au bablishi hufanya umeze hewa nyingi wakati w akutafuna au kumumunya, kuacha kufanya hivyo hupunguza kiwango cha hewa kinachoingia tumboni.
Acha kuvuta sigara
Hewa nyingi ikiwa Pamoja na hewa moshi ya sigara huingia tumboni wakati wa kuvuta sigara.
Jitibu magonjwa ya meno
Kama meno ni dhaifu na yamelegea huongeza hatari ya kumeza hewa ya ziada wakati wa kunywa au kutafuna.
Tembea baada ya kula
Kutembea hufanya misuli ya matumbo ya ndani nan je kujongea na hivyo kusaidia kutoa gesi tumboni baada ya kula.
Tibu kiungulia
Kutuliza kiungulia, unaweza kutumia dawa zadukani za kuzuia uzalishaji wa tindikali kwa muda.
Tibu kucheua tindikali
Kama una ugonjwa wa kucheua tindikali unaweza kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kwa muda, wakati unafnaya mpango wa kuonana na daktari kwa matibabu ya Zaidi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
25 Julai 2023 17:59:46
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Abraczinskas D. Overview of intestinal gas and bloating. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 23.07.2023
2. Cameron P, et al, Peptic ulcer disease and gastritis. In: Textbook of Adult Emergency Medicine. 5th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 23.07.2023
3. Feldman M, et al. Intestinal gas. In: Sleisenger and Fordtran's Gastrointestinal and Liver Disease: Pathophysiology, Diagnosis, Management. 10th ed. Saunders Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 23.07.2023
4. Gas in the digestive tract. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. https://www.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/gas-digestive-tract. Imechukuliwa 23.07.2023
5. Merck Manual Professional Version. Gas-related complaints. https://www.merckmanuals.com/professional/gastrointestinal-disorders/symptoms-of-gi-disorders/gas-related-complaints?query=gas-related complaints#. Imechukuliwa 23.07.2023
6. Rowland I, et al. Gut microbiota functions: Metabolism of nutrients and other food components. European Journal of Nutrition. 2018; doi:10.1007/s00394-017-1445-8.