top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

ULY CLINIC

13 Septemba 2023, 15:35:20

Kukojoa mara kwa mara
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kukojoa mara kwa mara

Kukojoa mara kwa mara husababishwa na nini

​

Kukojoa mara kwa mara ni hali ya kuhisi haja ya kwenda kukojoa zaidi ya kawaida yako, unaweza kuwa unakojoa kiwango kikubwa cha mkojo kuliko kawaida ama kiasi kidogo kidogo na mara nyingi.

​

Kukojoa mara kwa mara huweza kutokea wakati wa mchana au usiku tu au wakati wote yaani  usiku na mchana,  hii ina maana sana katika tiba na unatakiwa mwelezea daktari wako unakojoa mara kwa mara wakati gani.

 

Kukojoa mara kwa mara huweza kuathiri hali ya usingizi, kazi ama utu wako.

​

Visababishi ni nini?

 

Kukojoa mara kwa mara huweza kusababishwa na magonjwa yanayoathiri sehemu yoyote ile ya mfumo wa mkojo. Mfumo wa mkojo huhusisha figo, mirija ya mkojo (ureter) inayotoka kwenye figo mpaka kwenye kibofu, kibofu cha mkojo, na mrija unaotoa mkojo nje ya mwili (urethra)

 

Mambo mengi yanaweza kuambatanishwa na kukojoa mara kwa mara ni;

 

  • Maambukizi au magonjwa kwenye kibofu cha mkojo

  • Hali zinazoongeza uzalishaji mkojo kwa wingi

  • Mabadiliko katika misuli, mishipa ya fahamu ya kibofu cha mkojo

  • Matumizi ya dawa za kutibu saratani

  • Matumizi ya dawa na vinywaji vinavyoongeza uzalishaji wa  mkojo


Ikitegemea nini kinachosababisha kukojoa mara kwa mara, unaweza kupata dalili zingine kama

 

  • Maumivu au kupata shida wakati unakojoa

  • Kukojoa kwa kutumia nguvu

  • Kutoa mkojo kwa shida

  • Kushindwa kuzuia mkojo kutoka

  • Rangi ya mkojo kubadilika

 

Magonjwa  yanayosababisha kukojoa mara kwa mara ni haya yafuatayo;

 

​

ULY CLINIC inakushauri sikuzote utafute msaada kutoka kwa daktari wako mwenye weledi, anayetambulika na aliyesajiliwa na MCT mara utakapoona kuwa na dalili zinazoendana na makala hii kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ili upate tiba kulinganana tatizo lako halisi.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na Tiba kwa kupiga namba za simu au kubonyeza "Pata Tiba" chini ya tovuti hii.

​

ULY CLINIC pia inakushauri kwa urahisi wa kupata na kusoma makala zetu, weka app kwenye simu yako  kwa kubonyeza hapa

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

13 Septemba 2023, 15:35:20

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. MSD MANUAL Consumer Version. Urinary frequency. https://www.msdmanuals.com/home/kidney-and-urinary-tract-disorders/symptoms-of-kidney-and-urinary-tract-disorders/urination,-excessive-or-frequent?redirectid=11. Imechukuliwa 24.11.2020

2. Rakel RE, et al., eds. Urinary tract disorders.http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 24.11.2020.

3. LeBlond RF, et al., eds. The urinary system.http://www.accessmedicine.com. Imechukuliwa 24.11.2020

4. Web MD. Frequent micturition. https://www.webmd.com/urinary-incontinence-oab/frequent-urination-causes-and-treatments#. Imechukuliwa 24.11.2020

5. Health partner. https://www.healthpartners.com/blog/frequent-urination-in-women-12-causes-and-how-to-get-help/. Imechukuliwa 24.11.2020

bottom of page