top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

5 Novemba 2021, 10:20:14

Kung'ata ulimi usingizini
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Kung'ata ulimi usingizini

Kujing’ata ulimi wakati umelala huweza kutokea kwa mtu mwenye umri wowote ule, hata hivyo tafiti zinaonyesha, tatizo hutokea kwa watoto zaidi ukilinganisha na watu wazima. Majeraha mengine yanayoweza kuambatana na kujing'ata ulimi ni pamoja na kujing'ata kuta za ulimi(mashavu).

Makala hii imezungumzia kujing'ata ulimi wakati umelala(usiku) tu, kusoma kuhusu kujing'ata ulimi kusikotokea wakati wa kulala bonyeza hapa

Kuna sababu mbalimbali zinaweza sababisha mtu akajing;ata ulimi, zinaweza kuwa za kawaida au hali(tatizo) Fulani inayoendelea ndnai yamwili.

Visababishi

Baadhi ya visabaishi vinavyofahamika ni pamoja na ;

Tatizo la Kung’ata na kusaga meno(bruksizimu)

Hili ni tatizo la mijongeo ya misuli ya kinywa na taya, linaweza kutokea wakati ukiwa umelala haswa wakati unaota au kuamshwa kutoka usingizini. Tatizo hili husababisha maumivu ya misuli ya taya na kujijeruhi sehemu yoyote ile ya kinywa ikiwa pamoja na ulimi.

Degedegela la usoni

Degedege la misuli ya uso hutokea sana kwa watoto, degedege hili hupelekea kutetemeka kwa kidevu na kujing’ata ulimi wakati umelala

Matumizi ya dawa za kulevya

Dawa nyingi za kulevya husababisha furaha ya uongo kwa kusisimua mwili. Dawa hizi pia husababisha tatizo la kung’ata na kusaga meno wakati wa usiku kama lilivyoelezewa hapo juu. Mmea au dawa zitokanazo na mmea wa ectasy huonekana kusababisha sana tatizo hili na haifahamika kwanini.

Ugonjwa wa lyme

Huu ni ugonjwa unaofahamika vizuri, huathiri mfumo wa mijong'eo isiyo ya hiari pamoja na reflex katika sehemu mbalimbali za mwili ambayo huweza kupelekea kujing’ata ulimi wakati umelala. Hata hivyo dalili zingine huwa pamoja na kuhisi mkoleo wa baridiau joto lisilo la kawaida, uchovu mkali sana, kuongea kama mlevi, maumivu mwili mzima, kupata ganzi mwili mzima, kuharisha na kubadilika kwa uono wa macho.

Degedege wakati wa usiku

Degedege wakati wa usiku huweza kusababisha kujing’ata ulimi, hutokea sana kwa watu wenye tatizo la kifafa. Wagonjwa wa kifafa huweza kujing’ata ulimi wakiwa kwenye hali ya kupata degedege kwa sababu hupoteza fahamu wakati degedege linatoke. Wagonjwa hawa hujing’ata ulimi haswa kwenye kilele cha ulimi.

Madhaifu ya mijongeo ya misuli

Tatizo hili hutokea sana kwa watoto na hupelekea kujingata ulimi, wakati wa kutokea ni pale mtoto anapobebwa na usingizi. Mtoto huwa na mapozi tofauti tofauti ya kuchezesha kichwa, kurusha miguu na kubadili pozi la kiwiliwili bila hiari wakati wa kulala au akiwa usingizini. Hali hii huweza kusababisha pia tatizo la kujing’ata ulimi

Vihatarishi

Vihatarishi vya kujing'ata ulimi usingizini ni;


  • Kuwa na tatizo la ulimi mrefu- huweza kupelekea kujing’ata ulimi

  • Matumizi ya dawa za kulevya

  • Uvitaji wa sigara

  • Msongo wa mawazo wakati wa kulala

  • Kukosa hewa wakati wa usiku(apnea)

Dalili za kung’ata ulimi ukiwa umelala

  • Kutokwa na damu

  • Maumivu makali ya ulimi

  • Ulimi kuwa na rangi nyekundu

  • Kuonekana kwa alama ya mchaniko kwenye ulimi

  • Kidonda kwenye ulimi

Matibabu

Matibabu mara nyingi huhusisha kutibu kisababishi, wagonjwa wenye tatizo la kujing’ata na kusaga meno wakati wa usiku wanaweza kufaidika endapo watatumia mlinzi wa kinywa. Mlinzi wa kinywa ni kifaa maalumu kinachotumika kuzuia meno kusagana na kungata ulimi, hutolewa kwa daktari wa meno na hutengenezwa kulingana na maumbile ya kinywa cha mtu.

Matibabu mengine yanahusisha, kupunguza uzito, kuacha kuvuta sigara, kuacha kutumia dawa za kulevya, kutumia dawa za kifafa kama unatatizo la kifafa na endapo ni mgonjwa wa lyme unapaswa kuendelea na matibabu kama ulivyoelekezwa na daktari wako.

Endapo tayari umeshajing'ata matibabu ni yapi?

Ukiwa umeshapata tatizo la kijing’ata ulimi daktari anaweza kukupatia dawa za kutuliza maumivu pamoja na antibayotiki. Matibabu ya dawa za maumivu na antibayotiki hutegemea hali yako, haishauriwi kila mgonjwa kutumia antibayotiki ili kuzuia usugu wa dawa dhidi ya bakteria.

Ni lini jeraha langu la ulimi litapona?

Mara nyingi majeraha kwenye ulimi hupona haraka sana na bila kutumia dawa ndani ya wiki mbili, endapo utaona kuna kidonda endelevu, chekundu na kinatokwa na damu, usaha au kimechanika chanika tafuta msaada kutoka kwa daktari aiye karibu na wewe.

Kinga

Kinga ya kujing'ata ulimu usingizini ni;


  • Punguza msongo wa mawazo

  • Tumia kifaa maalumu cha kulinda kinywa chako

  • Usitumie dawa za kulevya

  • Tumia dawa zako ipasavyo endapo una ugonjwa wa kifafa, lyme

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

5 Novemba 2021, 10:28:35

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Kifafa. ULY CLINIC. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-kifafa. Imechukuliwa 18.07.2020

2. Willey online library. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/abs/10.1111/j.1600-0722.2004.00114.x. Imechukuliwa 18.07.2020

3. Epilepsy and behavior. Tongue bitting during in epileptic seizure. https://linkinghub.elsevier.com/retrieve/pii/S1525505012004507. Imechukuliwa 18.07.2020

4. RDH. Tongue chewing. https://www.rdhmag.com/pathology/oral-pathology/article/16406588/tongue-chewing. Imechukuliwa 18.07.2020

​5. WHO. Epilepsy. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/epilepsy. Imechukuliwa 18.07.2020

bottom of page