Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
3 Aprili 2020, 20:35:35
Leba halisi
Leba ni tendo la kifiziolojia ambalo linalomtoa mtoto pamoja na kondo la nyuma kutoka kwenye mfuko wa uzazi.
Leba halisi (uchungu halisi au uchungu wa uzazi) ni maumivu yasiyokoma yanayoongezeka kwa idadi na ukali na huambatana na maumivu ya nyuma chini ya mgongo, kubana kwa misuli ya mfuko wa uzazi na kufunguka kwa njia ya mlango wa uzazi.
Dalili za leba halisi (uchungu wa uzazi)
Maumivu ya kizazi yasiyokoma - Maumivu haya hayaishi kwa mazoezi mfano Kutembea.
Kubana kwa misuli ya uzazi kunakoongezeka makali jinsi muda unavyoenda.
Muda wa kukaza kwa uzazi huongezeka taratibu kwa idadi na makali.
Kiasi na muda wa kukaza na maumivu ya uzazi huongezeka kwa kasi
Huambatana na damu inayotoka ukeni iliyochanganyika na maji
Kupasuka kwa chupa ya uzazi( Mwanamke hutokwa na maji mengi ukeni yanayolowanisha chupi au kufika miguuni)
Kuanza kufunguka kwa mlango wa uzazi(seviksi)
Kuanza kushuka kwa mtoto kwenye tundu la uzazi
Maumivu huanza kwenye tumbo la uzazi hushuka kwa chini kuelekea kwenye sehemu za siri na mgongoni
Kuona mfuko wa amniotiki umetangulia ukeni
Dalili za leba isiyo halisi (uchungu usio usio wa uzazi)
Kubana kwa tumbo la uzazi kusikoongezeka kwa ukali na wingi jinsi muda unavyokwenda. Kubana huku huisha pia kwa mazoezi n.k
Maumivu ya tumbo huwa si makali sana
Maumivu huweza kuelekea nyuma ya mgongo
Maumivu ya tumbo juu ya kitovu
Vidokezo muhimu
Leba kwa kawaida hutokea kwa mama aliyefikisha wiki 37 na kuendelea za ujauzito.
Leba inayotokea kabla ya umri huu huitwa leba ya premature yaani leba inayotokea kabla yam toto kukomaa.
Leba ikitokea chini ya wiki 28 kwa Tanzania huitwa abosheni.
Leba inapoanza, huendelea kwenye hatua tatu kabla yam toto kutoka kwenye mfuko wa kizazi.
Hatua hizo zote ni za muhimu na muuguzi anapaswa kuwa karibu na mama mjamzito katika hatua zote akiendelea kuangalia maendeleo ya labor inavyokwenda.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.DC DUTTA'S textbook of obstetrics Ukurasa wa 116-121
2.ClevelandClinicFalseLabour& Pregnancy. https://my.clevelandclinic.org/health/articles/9686-true-vs-false-labor. Imechukuliwa 4/4/2020
3.WebMed DifferenceBtnFalseLabourAndTrueLabour. https://www.webmd.com/baby/qa/whats-the-difference-between-true-labor-and-false-labor. Imechukuliwa 4/4/2020
4.YouTubeVideo.DifferenceBtnFalseAndTrueLabour. https://www.youtube.com/watch?v=HVS2tFHP6Z4&app=desktop. Imechukuliwa 4/4/2020