Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sslome A, Md. Dkt. Sospeter B, MD
9 Februari 2024, 15:12:36
Macho mekundu
Ugonjwa wa jicho au macho mekundu ni tatizo linalojitokeza sana, huweza kuathiri jicho moja au macho yote na huweza kutokea katika mlipuko pia kulingana na ksiababishi. Hali hii hutokea pindi mishipa midogomidogo ya damu inapovimba au kupasuka kutokana na mambukizi au uchokozi (umwingiliano) katika jicho katika jicho.
Vyanzo vya kawaida vya jicho jekundu ni maambukizi na mzio na wakati mwingine huashiria tatizo kubwa la macho kama jeraha kwenye jicho, presha ya juu kwenye macho (glaukoma) n.k.
Hali ya macho mekundu huweza kuisha bila kuacha athari yoyote katika macho kwa matibabu ya nyumbani, hata hivyo ikiwa hali hii imeambatana na dalili kama kupungua kwa uono, maumivu makali, kuogopa mwanga nk unapaswa kupata msaada wa kitabibu.
Visababishi vya macho mekundu
Zifuatazo ni sababu za macho mekundu zinazojitokeza sana:
Maambukizi (hasa konjaktivaitisi na trakoma)
Mzio wa macho
Ukavu wa macho
Jeraha kwenye jicho
Kidonda kwenye Konea
Ugonjwa wa glaukoma
Sindromu ya kutumia kopmyuta
Dalili na viashiria vya macho mekundu
Dalili kuu ni rangi ya sehemu ya mbele ya jicho(konea) nyeupe ya jicho kuwa nyekundu, pia inaweza kuambatana na dalili pamoja na viashiria vifuatavyo kulingana na kisababishi;
Muwasho
Kutoa machozi
Macho kuuma
Kutoa tongotongo
Mabadilio ya kuona kama vile kuona ukungu
Kuvimba kwa macho
Mafua na kupiga chafya
Kikohozi
Kuvimba kwa tezi za tonsesi
Matibabu ya nyumbani
Ikiwa una macho mekundu na dalili za kawaida kama muwasho, maumivu kwa mbali, mafua, na kupiga chafya unaweza kujitibia nyumbani kwa kufanya yafuatayo;
Loweka kitambaa kizito katika maji ya baridi juu ya macho yaliyofungwa, husaidia kupunguza uvimbe na wekundu
Safisha macho yako kwa maji safi
Unaweza kutumia dawa za kawaida kupunguza dalili, mfano dawa za maumivu kama panadol, na za machozi bandia
Punguza matumizi ya vifaa vya kieletroniki kama vile kishikwambi na kompyuta
Punguza au acha matumizi ya vipodozi mpaka utakapopona
Ikiwa kisababishi ni mzio, fanya uchunguzi kubaini viamsha mzio na uviepuke
Ni wakati gani wa kumuona daktari?
Unatakiwa kumuona daktari endapo macho mekundu yameambatana na dalili hizi;
Unapata maumivu makali ya macho
Viepele usoni hasa eneo linalozunguka jicho
Umeanza kuwa na uono hafifu au kuona ukungu
Kutokwa na tongotongo zinazoganda kwenye kope
Macho mekundu baada ya upasuaji wa macho
Macho mekundu kwa mtu anayevaa lenzi bandia
Macho kuvimba
Una dalili zaidi ya wiki na zimekuwa zikiendelea kuwa mbaya
Macho mekundu yameanza baada ya kuumia jicho
Unapata maumivu ya kichwa na kutapika, na kuona ukungu
Jinsi ya kujikinga na macho mekundu
Unaweza kupunguza hatari ya kupata macho mekundu kwa kufanya yafuatayo:
Epuka kugusa au kufikicha macho yako na mikono michafu
Usitumie lenzi bandia zaidi ya muda ulioshauriwa
Safisha lenzi kama inavyopendekezwa
Ondoa lenzi wakati wa kulala
Ondoa vizuri urembo (make up) katika macho yako na hakikisha ni masafi
Usitumie vifaa kama simu au kompyuta kwa muda mrefu bila kupumzisha macho yako
Jitahidi kuepuka vitu vinavyoweza kusababisha macho kuwa na umwingiliano mfano moshi, vumbi nk
Mambo ya kuzingatia
Macho mekundu huweza kuashiria ugonjwa flani wa macho au kama dalili ya ugonjwa usiohusiana moja kwa moja na macho.
Macho mekundu yanaweza kupona kwa matibabu ya nyumbani, fika hospitali ikiwa una dalili za hatari kama maumivu na mabadiliko ya uono.
Usijaribu kutumia dawa za macho bila ushauri wa daktari.
Unaweza kuepuka macho mekundu kwa kuzingatia kanuni za usafi hasa eneo la uso.
Majina mengine
Majina mengine ya makala hii ni
Macho kuwa mekundu
Ugonjwa wa macho mekundu
Ugonjwa wa jicho jekundu
Dalili ya jicho jekundu
Tahadhari
Usitumie dawa yoyote kujitibu mwenyewe bila ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kusababisha kupoteza uono wa jicho.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
9 Februari 2024, 15:15:02
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. The red eye – first aid at the primary level - PMC – NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1705661/. Imechukuliwa 09.02.2024
2. The red eye – PMC. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3017259/. Imechukuliwa 09.02.2024
3. Red Eye - Eye Disorders - MSD Manual Professional Edition. https://www.msdmanuals.com/professional/eye-disorders/symptoms-of-ophthalmic-disorders/red-eye. Imechukuliwa 09.02.2024
4. Red Eyes: 20 Causes, Symptoms, Complications, and More. Healthline. https://www.healthline.com/health/eye-redness. Imechukuliwa 09.02.2024