Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
12 Aprili 2020, 16:50:51

Maumivu ya kifua, kifua kubana, kifua kuwa kizito
Kubana kwa kifua huwa ni ishara ya hali na magonjwa mbalimbali, baadhi ya magonjwa huwa ya hatari Zaidi, mfano magonjwa ya moyo na mapafu na baadhi huwa si ya hatari Zaidi.
Kifua kubana au kupata maumivu ya kifua haimaanishi moja kwa moja kwamba kuna shida kwenye mapafu, bali inamaanisha kuna tatizo lolote linaloweza kutokea kwenye mfumo wowote ndani ya mwili.
Pamoja na dalili ya kifua kubana, kuna dalili zingine zinazoweza kuambatana na zikapelekea daktari wako kujua ni nini hasa chanzo cha maumivu ya kifua au kifua kubana.
Baadhi ya sababu zinazopelekea kifua kubana na maumivu ya kifua ni;
Shambulio kwenye moyo (mshituko wa moyo)
Tatizo la woga na wasiwasi – ang’zayati
Ugonjwa wa gastroesofagio riflux
Kubana kwa misuli ya kifua
Nimonia(nyumonia)
Pumu ya kifua
Vidonda vya tumbo
Kuvunjika kwa mbavu
Kuvimba kwa kongosho
Shinikizo la juu la damu kwenye mapafu
Mawe kwenye mfuko wa figo
Magonjwa mbalimbali ya moyo
Kutanuka kwa misuli ya moyo kutokana na shinikizo la juu la damu
Moyo mkubwa(kutanuka kwa moyo)
Maambukizi kwenye mbavu- kostokondraitizi
Nyumothoraksi
Kuziba kwa mshipa ya damu ya moyo (koronari)
Kifua kikuu (TB)
Kumbuka
Kwa kila kisababishi kilichoorodheshwa hapo juu, zipo dalili zingine ambazo huelezea tatizo halisi, hapa chini dalili zingine zinazoambatana zimeelezewa kulingana na kisababishi halisi cha cha kifua kubana, kuwa kizito na kuwaka moto.
Shambulio kwenye moyo(mshituko wa moyo)
Mtu huyu huwa na dalili zifuatazo;
Maumivu makali ya katikati ya kifua ya kuchoma au kugandamiza
Maumivu yanayohamia taya la kushoto begani au mgongoni
Kifua kuwaka moto
Maumivu ambayo hubakia kwa dakika chache
Kichefuchefu
Kupumua kwa shida
Woga na wasiwasi (aang’zayati)
Mtu huyu huweza kuwa na dalili zifuatazo;
Kupumua kwa haraka
Kupumua kwa shida
Kizunguzungu
Misuli ya kifua kukaza
Ugonjwa wa gastroesofajio reflaksi (kucheua tindikali)
Ni hali ambayo hutokea pale ambapo Asidi kutoka tumboni hucheuliwa kwenye mrija wa esofagasi na koo, huambatana na dalili zifuatazo;
Kuhisi kifua kinachoma kama moto
Kushindwa kumeza
Kifua kuuma
Kubadilika kwa sauti
Maumivu ya katikati ya kifua yasiyohama
Kujongea kwa misuli
Licha ya kupelekea kifua kubana pia huweza kupelekea , maumivu, kuvimba kifua na shida wakati wa kupumua
Nimonia (homa ya mapafu)
Licha ya homa hii kupelekea kifua kubana pia hupelekea;
Maumivu ya kifua
Kuchanganyikiwa
Kukohoa
Kuchoka
Homa
Kichefuchefu
Pumu ya kifua
Pumu- licha ya kupelekea kifua kubana pia husababisha dalili zifuatazo;
Kupumua kwa shida
Kukohoa
Kupumua sauti zenye mlio kama filimbi
Vidonda vya tumbo
Huweza kupelekea kifua kubana na dalili zingine ambazo ni;
Maumivu ya tumbo yanayochoma
Kuhisi tumbo kujaa
Kiungulia ama kuchoma kwa kifua
Kichefuchefu
Kuvunjika mbavu
Hali hii hupelekea kifua kubana pamoja na dalili zingine kama maumivu kwenye kifua na kuhema kwa shida
Shinikizo la juu la damu la pulmonari
Ni moja ya hali ambayo hupelekea kifua kubana na dalili zingine ambazo ni;
Kupata shida kupumua
Kuchoka
Kizunguzungu
Kifua kuuma
Kifua kubana
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Health Line. Chest tightness. https://www.healthline.com/health/tight-chest. Imechukuliwa 12/4/2020
2.WebMd. Chest tightness. https://www.webmd.com/pain-management/guide/whats-causing-my-chest-pain. Imechukuliwa 12/4/2020
3.Mayo Clinic. Chest Pain. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/chest-pain/symptoms-causes/syc-20370838. Imechukuliwa 12/4/2020
4.Medical New Today cause of chest tightness. https://www.medicalnewstoday.com/articles/321650. Imechukuliwa 12/4/2020