top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin Lugonda, MD

17 Juni 2021, 11:47:37

Rangi ya  ute ukeni na maana yake kiafya
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Rangi ya ute ukeni na maana yake kiafya

Majimaji (ute) ya kawaida yanayotoka ukeni huzalishwa na tezi ndogo zinazopatikana kwenye tundu la uke na shingo ya kizazi.


Majimaji au ute huu hutoka kila siku ili kuondoa chembe zilizokufa na uchafu na kufanya uke uwe kwenye hali safi ya kiafya. Kiasi na rangi ya majimaji yatokayo ukeni hutofautiana kila siku na kwa kila mtu mmoja na mwingine. Kiasi na rangi ya majimaji yatokayo ukeni hutofautiana kila siku na kwa kila mtu mmoja na mwingine.


Makala hii imeelezea aina za ute na maana yake kiafya. Ute umetumika kumaanisha majimaji ya kawaida au uchafu unaoweza kutoka ukeni.


Je ni rangi gani za ute unaoweza kutoka ukeni?


Kuna rangi mbalimbali za ute unaoweza kutoka ukeni, rangi hizo ni;


  • Ute mweupe kama maziwa

  • Ute wa rangi ya maji

  • Ute wa rangi nyekundu

  • Ute wa rangi ya kijivu

  • Ute wa rangi ya kijani

  • Ute wa rangi ya njano

  • Ute wa rangi ya bluu


Kila rangi imeelezewa hapa chini ni nini kinaweza kuwa kisababishi


Ute mweupe rangi ya maji ukeni

  • Ute wa kawaida ukeni huwa na rangi kama ya maji kwa watu wengine huita uta mweupe lakini weupe si kama wa maziwa bali weupe wa maji. Licha ya kuwa mweupe kama maji, pia huwa na utelezi mithiri ya uterezi wa maji ya bamia au yai .

  • Ute ute huzidi kuteleza zaidi na kuwa mweupe zaidi kipindi cha hatari(kipindi yai linatolewa), wakati wa kusisimuliwa kingono na wakati wa ujauzito.


Ute wa rangi ya maziwa ukeni

Kutokwa na ute wa rangi nyeupe kama maziwa ukeni ni nini kisababishi?


  • Kutokwa ute wa rangi ya maziwa inamaanisha kutokwa na uchafu ulio mzito na mweupe kama maziwa au kuwa laini kama mafuta mgando(krimu).

  • Endapo ute huo hauambatani na dalili zingine ukeni, hii humaanisha ute wa kawaida kwa ajili ya kulainisha uke.

  • Endapo ute huu una harufu kali huweza kuashiria maabukizi ukeni na mara nyingi humaanisha maambukizi ya ‘fangasi ukeni’ ambapo huweza kupelekea dalili zingine za muwasho ukeni.


Ute wa rangi ya njano ukeni

Kutokwa na ute wenye rangi ya njano mpauko bila kuwa na dalili zingine humaanisha ute wa kawaida kwa ajili ya kulainisha uke na huweza kusababishwa pia mabadiliko ya chakula au matumizi ya virutubisho nyongeza.


Endapo ute una rangi ya njano iliyokolea au njano inayoelekea kijani, mara nyingi humaanisha maambukizi ya 'magonjwa ya zinaa'. Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni, harufu mbaya, kama ya kuoza samaki, majimaji kuwa mazito zaidi au mabonge.


Ute wa rangi nyekundu ukeni

  • Ute wa rangi nyekundu huweza kuwa na wekundu mpauko au mkoleo ama rangi ya kutu. Mara nyingi ute wa rangi nyekundu husababisha na hedhi.

  • Endapo ute unatoka ndani ya siku za hedhi kila mwisho wa mwezi yaani kila baada ya siku 28 hadi 35 kutoka mzunguko mmoja hadi mwingine hii humaanisha ute wa kawaida baada au kabla ya hedhi.

  • Endao ute wa rangi hii unatoka katikati ya mzunguko wa hedhi, hii mara nyingi huashiria matatizo mbalimbali kama matatizo ya homoni, saratani ya shingo ya kizazi n.k

  • Endapo ute mwekundu unaambatana na harufu kali ukeni na katikati ya hedhi au kwenye hedhi, maranyingi ina maanisha dalili za awali za saratani ya shingo ya kizazi.

  • Endapo upo kwenye koma hedhi kipindi angalau mwaka mmoja mfululizo na unatokwa na majimaji ya rangi nyekundu ukeni, inaweza kumaanisha saratani ya mji wa uzazi, au saratani ya shingo ya kizazi.


Ute wa rangi ya pinki ukeni

Ute wa pinki unaweza kuwa pinki mpauko au ile iliyokolea, hii husababishwa mara nyingi na uwepo wa damu kidogo.


Kutokwa na ute wa rangi ya pinki humaanisha unakaribia kuingia hedhi na endapo umeshika ujauzito, humaanisha upo kipindi cha upandikizaji wa yai lililochochavushwa mwanzoni kabisa mwa ujauzito.


Baadhi ya wanawake wakiwa siku za hatari (yai linapotolewa), hupata matone ya damu kidogo yanayoweza kupelekea ute ukeni kuwa na rangi ya pinki ambayo ni kawaida.


Ute wa pinki pia unaweza kutokea baada ya kushiriki ngono na umepata majeraha kidogo kwenye uke yaliyosababisha damu kuvia na hivyo ikachanganyika na kusababisha majimaji kuwa na rangi hiyo ya pinki.


Ute wa rangi ya kijivu ukeni

Kutokwa na ute wa rangi ya kijivu si kawaida na huweza maanisha mara nyingi maambukizi ya bakteria ukeni haswa ugonjwa wa vajinosis ya bakteria. Dalili zinazoambatana na ute au uchafu huu wa rangi ya kijivu ukeni na kumaanisha maambukizi ya bakteria ni miwasho, michomo, harufu kali kuwa na wekundu maeneo yanayozunguka mashavu na tundu la uke.


Ute wa rangi ya kijani ukeni

Kutokwa na ute wa rangi ya kijani au njano kijani ukeni mara nyingi huashiria maambukizi ya 'magonjwa ya zinaa'. Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni harufu mbaya au kama samaki aliyeoza, ute kuwa mazito zaidi au kama mabonge.


Wakati gani unapaswa kuwasiliana na daktari haraka?


Endapo unatokwa na uchafu(ute) ukeni unaoambatana na dalili zifuatazo tafuta msaada wa daktari.


  • Kujihisi hali isiyo kawaida ukeni

  • Kutokwa na damu wakati wa kushiriki ngono

  • Kutokwa na damu katikati ya vipindi vya hedhi

  • Kutokwa na damuu baada ya komahedhi

  • Kutokwa na harufu mbaya ukeni kama ya kitu kilichooza (samaki)

  • Kutokwa na ute wa rangi ya kijani, njano au kijivu

  • Kutokwa na ute wenye povu

  • Maumivu

  • Muwasho wa uke

  • Uchafu ukeni unaoambatana na hisia za kuungua wakati wa kukojo


Wapi utapata taarifa zingine zaidi?


Soma zaidikuhusu


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

31 Desemba 2021, 05:49:04

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. 5 Types of vaginal discharge & what they mean.
https://www.unitypoint.org/livewell/article.aspx?id=06f8f035-9f6e-4a79-bb58-9045b9d7d0d8. Imechukuliwa 16.06.2021

2. Merck manual. Vaginal discharge. https://www.merckmanuals.com/home/women-s-health-issues/symptoms-of-gynecologic-disorders/vaginal-discharge. Imechukuliwa 16.06.2021

3. Vaginal discharge. http://www.pamf.org/teen/health/femalehealth/discharge.html. Imechukuliwa 16.06.2021

4. Vaginal discharge. https://familydoctor.org/condition/vaginal-discharge/. Imechukuliwa 16.06.2021. Imechukuliwa 16.06.2021

5. Vaginal discharge. https://www.hhs.gov/opa/reproductive-health/fact-sheets/vaginal-discharge/index.html. Imechukuliwa 16.06.2021

6. Vaginal discharge. https://www.sutterhealth.org/health/teens/female/vaginal-discharge. Imechukuliwa 16.06.2021

7. Vaginal discharge.https://www.drugs.com/health-guide/vaginal-discharge.html. Imechukuliwa 16.06.2021

8. What's the cervical mucus method of FAMs?. https://www.plannedparenthood.org/learn/birth-control/fertility-awareness/whats-cervical-mucus-method-fams. Imechukuliwa 16.06.2021

bottom of page