Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
12 Aprili 2020, 17:30:46
Saratani ya ziwa
Saratani ni mkusanyiko wa magonjwa unaohusisha uzalishwaji wa seli zisizo rasmi na usiozuilika sehemu yeyote katika mwili wa binadamu.
Mara nyingi uzalishwaji wa seli za saratani huwa hauna mwisho na huwa endelevu. Uundwaji hovyo wa seli husababisha uvimbe katika mwili wa binadamu ambao hukua na kupelekea kubanwa kwa mishipa ya damu, ubongo, mifupa, neva, ini na ogani nyingine nyingi.
Saratani husababisha kifo baada ya kupitia kipindi cha maumivu makali.
Kuna saratani zinazosababishwa na virusi mfano saratani ya shingo ya kizazi na saratani ambazo hazifahamiki visababishi.
Saratani ya ziwa ni uundwaji usio rasmi na usiozuilika wa seli za ziwa/titi na mara nyingi huanza katika seli za mirija inayotengeneza maziwa. Saratani ya ziwa hutokea kwa wanawake mara nyingi zaidi ya wanaume.
Saratani ya ziwa inaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kupitia kwenye mishipa ya damu na mishipa ya limfuna kuathiri sehemu nyingine za mwili. Wakati mwingine saratani inaposafiri na kujishikiza sehemu nyingine ya mwili, hukua pale na kuleta madhara.
Vihatarishi
Vilivyoorodheshwa hapa chini ni vihatarishi vya kupata saratani kutokana na tafiti zilizofanyika, sio lazima kila mwenye kihatarishi anaweza kupata saratani, kuna baadhi ya watu huwa hawana vihatarishi lakini wanapata saratani ya ziwa.
Kuwa mwanamke -mara nyingi wanawake ndio wanaathirika sana kuliko wanaume
Kurithi- hii hutokana na kurithi vinasaba vya ugonjwa kutoka kwa wazazi
Familia kuwa na historia ya saratani ya ziwa- kama kuna mwanafamilia aliyewahi kupata saratani ya ziwa basi kunauwezekano mkubwa wa kupata saratani hiyo
Umri mkubwa- athari za kupata saratani ya ziwa huongezeka zaidi kadiri umri unavyozidi kuongezeka
Kupata mtoto ukiwa na zaidi ya miaka 35
Uzito mkubwa
Kutokufanya mazoezi
Mwanamke ambaye hajawahi kupata ujauzito ana hatari kubwa ya kupata saratani ya ziwa kuliko Yule aliyewahi kupata ujauzito.
Uvutaji sigara na
Matumizi ya pombe
Dalili
Uvimbe au ngozi ngumu ndani au karibu na titi au chini ya kwapa
Mabadiliko ya umbo au ukubwa wa titi moja au yote mawili
Mabadiliko ya rangi au umbo la chuchu
Ngozi ya titi kujikunja au kuwa na makunyanzi
Chuchu ya titi kudidimia ndani au kuingia kwa ndani
Kutokwa na majimaji, usaha au damu kwenye chuchu
Ngozi ya titi kuwa nyekundu na kuwa na magamba (kama ganda la chungwa)
Maumivu ya titi au chuchu
Kuwashwa kwa chuchu
Kuhisi uvimbe ndani ya ziwa
Kuwashwa kwa titi
Kuhisi titi kuwa gumu, kuuma au kuwa na joto sana ukishika
Kuongezeka ukubwa kwa uvimbe ndani ya chuchu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023, 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1)Definition of cancer at https:// www.medinenet.com/cancer/article.htm# what is cancer. Imechukuliwa 9/4/2020
2)CDC. Breast cancer definition at https://www.cdc.gov/cancer/breast/basic_info/index.htm . Imechukuliwa 9/04/2020
3)Mayo clinic. Breast cancer. https://www.mayoclinic.org/disease-conditins/breast-cance/symptoms-causes/syc-20352470. Imechukuliwa 09/04/2020
4)Cancer treatment centre for America. Breast cancer symptoms. https://www.cancercenter.com/cancer-types/breast-cancer/symptoms. Imechukuliwa 9/04/2020