top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

17 Desemba 2024, 06:06:59

Shinikizo la juu la damu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Shinikizo la juu la damu

Shinikizo la damu la juu ni hali inayotokea endapo msukumo ndani ya mishipa ya damu imezidi kiwango cha kawaida kinachofanhamika kiafya ambacho ni 139/79 mmHg. Kuzidi kwa msukumo hunaweza sababishwa na hali na magonjwa mbalimbali. Ili tuweze kujua kuhusu shinikizo la damu la juu ni vema kwanza kujua aina za shinikizo la damu la juu.


NB: Kwenye makala hii neno shinikizo la juu la damu hufahamika kwa majina mengine ya kupanda kwa presha ya damu, au kupanda kwa shinikizo la damu.

​

Aina za shinikizo la juu la damu

Tatizo la kupanda kwa shinikizo la damu limegawanyika katika makundi makuu mawili. Shinikizo la juu awali na Shinikizo la juu la upili

​

Shinikizo la juu la awali: Kisababishi mara nyingi hakifahamika na huchangia kwa asilimia 90 hadi 95 ya ugonjwa huu kwa haswa watu wazima wenye umri kati ya miaka 35 na kuendelea.


Aina hii ya shinikizo huhusianishwa na sababu za kimazingira au za kiasilia kama ifuatavyo;


  • Kurithi- inaonekana kwamba watu wengi wenye shinikizo la damu baadhi huwa na historia hii kwenye familia zao lakini  urithishwaji huu bado haueleweki vizuri. Kuna utafiti umefanyika na kuonesha watoto mapacha wanaozaliwa wote wanaweza kupata shinikizo la damu la juu kwa asilimia 33-57%

  • Unene wa kupindukia (Obeziti)

  • Ugonjwa wa kisukari

  • Magonjwa ya moyo


Shinikizo la juu la upili: Linachangia kwa asilimia 5-10 kusababisha shinikizo la juu la damu na hutokea sana kwa watu wenye umri chini ya miaka 35. Zipo sababu za moja kwa moja zinazofahamika kusababisha aina hii ya shinikizo.

​

Shinikizo la juu la damu linalozidi la 180/120 linaweza kugawanywa tena katika makundi mawili ambayo ni;


  • Shinikizo la damu la juu linalohitaji matibabu ya haraka

    • Shinikizo hili haliambatani na ishara ya kuharibika kwa ogani ndani , mgonjwa huenda hospitali akiwa anajihisi vibaya na anapopimwa anakuwa na shinikizo la juu sana. Matibabu ya shinikizo hili huchukua siku mbili hadi tatu kwa matumizi ya dawa za kumeza mgonjwa akiwa amelazwa wodini, au nyumbani chini ya usimamizi wa daktari.

​

  • Shinikizo la damu linalohitaji matibabu ya dharura

    • Aina hii huwa inajitokeza na dalili za uhalibifu wa organi mbalimbali mwilini kama vile macho(kushindwa kuona vema), ubongo( mabadiliko ya kiakili/tabia ya mtu), figo (kutokukojoa au kukojoa mkojo kidogo sana), mapafu(maumivu ya kifua) na moyo(maumivu ya moyo ya ghafla na maumivu ya kifua), mapafu (maji kwenye mapafu) na ujauzito( kifafa cha mimba), ubongo ( damu kuvia kwenye ubongo) na moyo (mshituko wa moyo na kifo)

    • Mgonjwa anahitaji matibabu ya dharura kwenye chumba cha watu mahutui yani ICU na matibabu yake yanahusisha kushusha shinikizo hili ndani ya saa 1 au 2 kwa dawa za mishipa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kuokoa maisha.

Dalili za shinikizo la juu la damu

Mara nyingi shinikizo la juu la damu huwa halina dalili kwa watu wengi, endapo zitatoke, huwa miongozi mwa zifuatazo:


  • Maumivu ya kuchwa

  • Kuishiwa pumzi

  • Kutokwa damu puani


NB: Kutokea kwa dalili hizi hazimaanishi una shinikizo la juula damu kwa kuwa huweza kusababishwa na matatizo mengine. owever, dalili hizi zikitokea humaanisha shinikizo limekuwa kubwa kutishia uhai wa mtu.


Je, kuna mahusiano ya vyakula na mfumo wa maisha na shinikizo la damu la juu?


Ndio kuna mahusiano makubwa ya shinikizo la damu na chakula. Pengine mtu mwenye dalili za kuanza kupata shinikizo au mwenye shinikizo anashauriwa kubadili mfumo wa maisha yake kama ifuatavyo;

​

  • Punguza kula vyakula vya mafuta kwa wingi hasa vyenye lehamu mbaya ili kuzuia magonjwa ya moyo

  • Tumia chumvi kiasi kinachoshauriwa kiafya kulingana na hali yako ( Inapendekezwa kutumia chini ya miligramu 2300 kwa siku ikitegemea na hali yako

  • Ongeza kula vyakula vya matunda na mboga mboga

  • Kula vyakula vyenye madini ya kalisiamu kwa wingi kama viazi vitamu, ndizi n.k

  • Acha kuvuta sigara

  • Fanya mazoezi kwa angalau  dakika 30 kila siku utazuia ongezeko la uzito na magonjwa ya moyo

  • Puguza uzito

  • Punguza msongo wa mawazo

  • Kuwa na tabia ya kupima shinikizo la damu kila mwezi ili kujua shinikizo lako la damu. Itakusaidia kutambua mapema kama likibadilika

  • Tumia dawa kila siku endapo umeanzishiwa dawa za kushusha shinikizo la damu ili kuepuka madhara yake.


Mwone dakitara mara unapopata tatizo lolote ambalo hulielewi

​

Soma hapa kuhusu kushusha shinikizo la damu pasipo kutumia dawa


Hatua za shinikizo la damu

​

Haipatensheni imegawanywa kwenye makundi mengine mawili kulingana na  kiwango cha shinikizo la damu.

 

Shinikizo la damu la kawaida ambalo ni

 

SBP/DBP   120/80 mmHg

 

Shinikizo la damu linaloelekea kupanda

 

SBP/DBP   120-138/80-90 mmHg

 

Shinikizo la damu la juu kundi la kwanza

 

140-159/90-99

 

Shinikizo la damu la juu kundi la pili

 

SBP 160mmHg au zaidi na DBP kuwa 100mmHg au zaidi milimteter za mercury


Mgawanyo huo hutokana na vipimo viwili au zaidi kila unapoenda kupimwa hospitali na dakitari. Kwa maana nyingine unapoenda kupimwa kwa mara ya kwanza na kukutwa na shinikizo la damu la juu haiwezi kuita unashinikizo la damu la juu mpaka umepima vipimo mara mbili siku tofauti na kukutwa na shinikizo hilo la juu.


Nini husababisha shinikizo la damu la juu?

​

Shinikizo la juu la upili husababishwa na magonjwa malimbali yafuatayo;

​

  • Magonjwa ya figo

    • Ugonjwa wa vifuko vya maji ndani ya figo

    • Magonjwa sugu ya figo

    • Kuziba kwa mija wa mkojo kwa mda mrefu kama( urethra)

    • Saratani inayozalisha homoni ya renini kwa wingi

 

  • Magonjwa ya mishipa ya damu

    • Magonjwa ya Aota ama koaktesheni ya aota​

    • Anurizimu ya aota

    • Ugonjwa wa kusinyaa kwa mishipa ya figo (reno-stenosisi)

 

  • Matatizo/mabadiliko ya kwenye vichochezi vya mwili kama vile​​:

    • Sindromu ya kushing husababisha uzalishaji mwingi au matumizi ya dawa kundi  la glucocorticoid kwa muda mrefu

    • Kuzalishwa kwa wingi kwa vichocheo mwili aina ya aldosterone

  • Mtoto kuzaliwa na tezi kubwa ya adreno

  • Saratani ya tezi ya adreno  iitwayo fiokromosaitoma

 

  • Matatizo ya mfumo wa fahamu kama vile

    • Saratani ya ubongo

    • Shinikizo la damu la kwenye ubongo

 

  • Dawa na sumu ambazo ni

    • Pombe

    • Kokaine

    • Baadhi ya dawa za saratani

    • Dawa aina ya asprini

    • Nikotini

    • Baadhi ya dawa za kienyeji

    • Homoni  ya adrenalini


  • Sababu nyinginezo

    • Ujauzito

    • Kuzidi kwa madini ya kalisium mwilini

    • Kiwango cha juu au chini cha vichochezi mwili vya tezi ya thairoid au

    • Kiwango cha juu au chini cha vichochezi mwili vya tezi ya parathairoidi

    • ugonjwa wa slipu apnia.

 

 

Nini husasabisha shinikizo la juu la damu linalohitaji matibabu ya haraka?

 

Wagonjwa wengi wenye tatizo kama hili huwa wana shinikizo la juu la damu na wameacha kutumia dawa ghafla au dawa walizokuwa wanatumia zilikuwa hazikidhi mahitaji na hivo kuisha au kushindwa kudhibiti shinikizo la damu. Shinikizo la damu hupanda kwa haraka endapo dawa hazitumiwi ipasavyo au hazifanyia kazi.

​

Mambo mengine yanayoweza kusabaisha tatizo hili ni kufanyiwa upasuaji wa kutoa saratani ya  pheochromocytoma, magonjwa ya figo kama vile Glomerunonefraitizi, ugonjwa wa mishipa ya figo, magonjwa yanayotokana vichochezi mwili n.k kama ilivyoelezewa hapo juu.


​Je vipimo gani nitafanyiwa hospitali?

Vipo vipimo vya aina nyingi na hutegemea dalili ulizonazo lakini vipimo hivi huweza kufanyika;

​

  • Kipimo cha kupima shinikizo la damu la juu

  • Kipimo cha mkojo au damu kuangalia kazi ya figo na ini na vitu vingine

  • Kipimo cha mionzi (x-ray)

  • Kipimo cha CT scan

  • Kipimo cha angiografi ya Figo na Mshipa wa aota

  • Kipimo cha Kolestro kwenye damu

  • Kipimo cha elekrolaiti kwenye damu kama Sodiamu na kalisimau

  • N.k

 ​

Je kuna matibabu ya ugonjwa huu?

 

Matibabu ya haipatensheni  yapo na ni ya muda mrefu. Dakitari anaweza kuamua kukuanzishia matibabu kulingana na kiwango cha  shinikizo lako la damu na kukushauri kubadilisha mfumo wa maisha yako. 

​

Soma kuhusu malengo ya kushusha shinikizo la damu ili kujua shinikizo lako ni la kawaida au la wa kubonyeza hapa


ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

17 Desemba 2024, 06:56:25

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

High blood pressure. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health/high-blood-pressure. Imechukuliwa 10.12.2024

Flynn JT, et al. Clinical practice guideline for screening and management of high blood pressure in children and adolescents. Pediatrics. 2017; doi:10.1542/peds.2017-1904.

Physical Activity Guidelines for Americans. 2nd ed. U.S. Department of Health and Human Services. https://health.gov/our-work/physical-activity/current-guidelines. Imechukuliwa 10.12.2024

Hypertension in adults: Screening. U.S. Preventive Services Task Force. https://uspreventiveservicestaskforce.org/uspstf/recommendation/hypertension-in-adults-screening. Imechukuliwa 10.12.2024

Thomas G, et al. Blood pressure measurement in the diagnosis and treatment of hypertension in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 10.12.2024

Muntner P, et al. Measurement of blood pressure in humans: A scientific statement from the American Heart Association. Hypertension. 2019; doi:10.1161/HYP.0000000000000087.

Basile J, et al. Overview of hypertension in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 10.12.2024

Know your risk factors for high blood pressure. American Heart Association. https://www.heart.org/en/health-topics/high-blood-pressure/why-high-blood-pressure-is-a-silent-killer/know-your-risk-factors-for-high-blood-pressure. Imechukuliwa 10.12.2024

Rethinking drinking. Alcohol and your health. National Institute on Alcohol Abuse and Alcoholism. https://www.rethinkingdrinking.niaaa.nih.gov/Default.aspx. Imechukuliwa 10.12.2024

Libby P, et al., eds. Systemic hypertension: Mechanisms, diagnosis, and treatment. In: Braunwald's Heart Disease: A Textbook of Cardiovascular Medicine. 12th ed. Elsevier; 2022. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.12.2024

AskMayoExpert. Hypertension (adult). Mayo Clinic; 2021.
About metabolic syndrome. American Heart Association. https://www.heart.org/en/health-topics/metabolic-syndrome/about-metabolic-syndrome. Imechukuliwa 10.12.2024

Understanding blood pressure readings. American Heart Association. https://www.heart.org/en/health-topics/high-blood-pressure/understanding-blood-pressure-readings. Imechukuliwa 10.12.2024

Whelton PK, et al. 2017 ACC/AHA/AAPA/ABC/ACPM/AGS/APhA/ASH/ASPC/NMA/PCNA guideline for the prevention, detection, evaluation, and management of high blood pressure in adults: A report of the American College of Cardiology/American Heart Association Task Force on Clinical Practice Guidelines. Hypertension. 2018; doi:10.1161/HYP.0000000000000065.

Monitoring your blood pressure at home. American Heart Association. https://www.heart.org/en/health-topics/high-blood-pressure/understanding-blood-pressure-readings/monitoring-your-blood-pressure-at-home. Imechukuliwa 10.12.2024

bottom of page