Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
14 Septemba 2023, 17:13:09
Tumbo kujaa gesi na kuvuruga
Dalili hii ya tumbo kujaa gesi mara nyingi husababishwa na ulaji wa vyakula vya aina fulani, hata hivyo kuna baadhi ya matatizo ya kiafya yanayoweza kusababisha tatizo hili.
Ingawa watu wengi hufahamu kwamba tumbo kujaa gesi husababishwa na kula maharagwe, ama vitunguu, ni muhimu kutambua kwamba kuna sababu zingine pia ambazo zinajumuisha ulaji wa vyakula vilivyoorodheshwa hapa chini;
Vyakula vinavyosababisha tumbo kujaa gesi
Ulaji wa vyakula vyenye maziwa au maziwa
Matunda aina kadhaa yenye gesi kwa wingi kama vile tufaa, tikiti maji na peasi
Soda viazi vitamu na viazi mviringo
Mahindi ya kuchemsha au kuchoma
Pilau
Sukari aina ya fructose inayopatikana kwenye matunda na soda, lactose inayopatikana katika maziwa au vyakula vyenye mazao ya maziwa na vyakula vya kusindikwa huwa visababishi vikuu vingine vya tumbo kujaa gesi, maumivu ya tumbo, na kuhara
Dalili zingine zinazoweza kuambatana na tumbo kujaa gesi na kuvuruga ni;
Kuhisi mvurugiko wa tumbo
Kuhisi sauti za mijongeo ya tumbo
Kubeua mara kwa mara
Maumivu ya tumbo
Visababishi
Katika sehemu hii utajifunza visababishi vingine vya tumbo kujaa gesi mbali na vyakula ambacho ni kisababishi kikuu
Tatizo la tumbo kujaa gesi pia linaweza kusababishwa na magonjwa yafuatayo;
Ugonjwa wa syndrome ya Irritable bowel
Ugonjwa huu hutokea kutokana na mvurugiko wa mfumo wa tumbo, huwa ni vigumu sana kugunduliwa na dakitari kwa sababu dalili zake hufanana na magonjwa mengine.
Dalili zifuatazo huweza kuambatana na ugonjwa huu;
Tumbo kujaa gesi
Kuvimba kwa tumbo
Kuhisi mvurugiko wa tumbo
Kukosa choo kwa muda wa wiki moja na kufuatiwa na kuhara wiki inyofuata
Hakuna kisababishi halisi kinachosababisha ugonjwa huu ila kuna vihatarishi vinavyofahamika vinachangia kuamsha tatizo hili kama vile
Kuharibika kwa mfumo wa vichochezi mwili
Kuharibika kwa mfumo wa fahamu wa ubongo
2. Kiungulia
3. Maambukizi ya giardia
4. Matumizi ya baadhi ya dawa
5. Kuongezeka uzito
6. Magonjwa ya akili kama msongo wa mawazo, shauku kuu na sononeko
7. Magonjwa ya kula kama anoreksia nevosa na bulimia nevosa
8. Mwili Kutohimili vyakula vya laktosi
Matibabu
Matumbo ya mtu huwa hayana tatizo lolote na mwathilika huwa mzima katika mfumo wa chakula, dalili za ugonjwa huu mara nyingi huwa mbaya wakati wa jioni. Cha kusikitisha ni kwamba hakuna tiba kwa ajili ya kuondoa kabisa tatizo hili, kinachofanyika ni kupunguza dalili na kubadili mfumo wa maisha tu.
Matibabu ya nyumbani
Punguza vyakula vya nyuzinyuzi zinazotokana na vyakula vya mbegu huweza kusaidia kupunguza dalili za tatizo hili kwa asilimia 20 hadi 30
Zuia kula mikate, mayai, ngano, biskuti , vitumbua, maandazi na vyakula vingine jamii ya ngano.
Zuia vyakula vingine kama mayai au vyakula vyenye mayai kwa sababu huleta gesi
Zuia kula vitu vifuatavyo kama utaweza, ngano, vitunguu, kabeji, alizeti, maharagwe, tufaa,tikiti maji, peasi,
Zuia kutafuna bigijii ili kuepuka kumeza gesi
Tafuna chakula taratibu kuzuia kumeza gesi, pia usile mlo mkubwa kwa wakati mmoja
Zuia kumeza chakula na maji ili kuepuka gesi kuingia tumboni
Tumia vyakula visivyo na maziwa au mazao ya maziwa
Fanya masaji ya tumbo kukusaidia ubeue gesi iliyo tumboni
Tumia dawa za kusaidia mmeng'enyo wa vyakula vya laktozi na gluteni
Zuia kupata haja ngumu au kukosa haja kubwa kwa muda mrefu, tumia vyakula vya kulainisha tumbo na kunywa maji ya kutosha oamoja na kufanya mazoezi
Ongea na daktari wako kuhusu kutumia dawa za antibayotiki endapo gesi yako inasababishwa nabakteria kwenye tumbo
Tumia mafuta yenye minti (kuzuia) kupata gesi
Onana na daktari wako endapo umefanya matibabu ya nyumbani pasipo kupata nafuu yoyote ndani ya wiki moja
Wakati gani uwasiliane na daktari unapokuwa na hali hii?
Mwone daktari wako endapo unapata dalili ya tumbo kujaa gesi pamoja na;
Maumivu makali ya tumbo na endelevu
Unapata damu kwenye choo, kupata choo cheusi au kinachonata kama lami
Unapata homa kali
Kuharisha
Kuzidi kwa kiungulia
Kutapika
Kupoteza uzito bila sababu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
14 Septemba 2023, 17:13:09
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
Thiwan S. (n.d.). Abdominal bloating: A mysterious symptom.
med.unc.edu/ibs/files/educational-gi-handouts/Abdominal%20Bloating.pdf. Imechukuliwa 29.06.2020
Wang TJ, et al. (2020). The effect of abdominal massage in reducing malignant ascites symptoms.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/25558030. Imechukuliwa 29.06.2020
Functional GI disorders. (2020). iffgd.org/functional-gi-disorders.html. Imechukuliwa 29.06.2020
Gas. (2018). my.clevelandclinic.org/health/diseases_conditions/hic_Gas. Imechukuliwa 29.06.2020
Mayo Clinic Staff. (2020). Bloating, belching and intestinal gas: How to avoid them.
mayoclinic.org/diseases-conditions/gas-and-gas-pains/in-depth/gas-and-gas-pains/art-20044739. Imechukuliwa 29.06.2020
Seo AY, et al. (2020). Abdominal bloating: Pathophysiology and treatment.
jnmjournal.org/journal/view.html?uid=327&vmd=Full. Imechukuliwa 29.06.2020