top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter Mangwella, MD

12 Juni 2021, 19:25:17

Vichomi vya tumbo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Vichomi vya tumbo

Vichomi vya tumbo katika Makala hii inamaanisha maumivu makali, yanayotokea ghafla na kudumu kwa sekunde chache kisha kupotea. Visababishi vya maumivu ya tumbo yanayodumu zaidi ya muda huu vimeandikwa kwenye makala nyingine ya ‘Maumivu ya tumbo’


Kichomi tumboni husababishwa na;


  • Vifuko maji vya ovari

  • Gastroenteraitiz

  • Sumu ya chakula

  • Kutostahimili laktosi

  • Kuvimbiwa

  • Maambukizi ya UTI

  • Mawe ya kibofu nyongo

  • Michomo ya kidole tumbo

  • Sindromu ya iritabo bawel

  • Ujauzito nje ya kizazi

  • Matatizo ya mfumo wa uzazi

  • Vidonda vya tumbo

  • Maambukizi ya virusi tumboni

  • Maumivu ya hedhi

  • Uchungu wa uongo


Michomo ya kidole tumbo

Michomo ya kidole tumbo kwa jina lingine hufahamika kama apendisaitiz, hutokana na mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya maambukizi ya bakteria kwenye kidole tumbo inayowezwa kuamshwa na kuziba kwa kidole tumbo.


Maumivu ya michomo ua kidole tumbo huwa na sifa ya kuanza kwenye kitovu, na kisha kuelekea eneo la chini ya kitovu kulia mwa tumbo. Maumivu yanaweza kuwa makali sana na kupotea au kudumu kwa sekunde kadhaa. Awali maumivu yanaweza kuja na kuondoka kwa muda mfupi lakini tatizo linapoendelea maumivu huweza kudumu kwa muda mrefu. Kuna dalili zingine ambazo huambatana na tatizo hili kama vile kichefuchefu n.k. Soma zaidi Makala ya michomo kwenye kidole tumbo.


Michomo ya kongosho

Michomo ya kongosho kwa jina jingine huitwa pankriataitiz, hutokana na mwitikio wa kinga ulinzi wa mwili dhidi ya vhichokozi vya kongosho kweye tezi kongosho. Vichokozi vinaweza kuwa, pombe, upasuaji wa tumbo, matumizi ya aina fulani ya dawa n.k.


Dalili za michomo ya kongosho ni maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na kichefuchefu na kutapika.


Gastroenteraitiz

Maambukizi ya bakteria au virusi kwenye tumbo huweza pelekea maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na kichefuchefu, kutapika na kuharisha.


Kuziba kwa utumbo

Vitu vingi vinaweza kusababisha kuziba kwa utumbo na kupelekea maumivu ya tumbo yaliyo makali kutokana na kutosafiri vema kwa chakula na maji tumboni. Kuziba huku huweza sababishwa na makovu ya upasuaji au magonjwa ya tumbo au kujikunja kwa utumbo. Kuziba kwa tumbo hupelekea sehemu husika ya utumbo kukosa damu, hii hupelekea kutokea kwa maumivu makali ya tumbo, endapo tatizo linaendelea, maumivu ya tumbo nayo huendelea kwa muda mrefu na matibabu ya dharura huhitajika.


Majeraha ya tumbo

Majeraha ya moja kwa moja kutokana na ajali, kuangukia tumbo au kupigwa tumboni huweza pelekea kupasuka au kuchanika kwa mishipa na ogani mbalimbali ndani ya tumbo na hivyo kuambatana na maumivu makali ya tumbo. Ogani ndani ya tumbo ambazo hupasuka au kuchanika kirahisi kutokana na ajali hata kama ni ndogo ni ini na bandama. Maumivu ya kuchanika au kupasuka kwa ogani ndani ya mwili huhitaji matibabu ya dharura.


Maumivu ya daivetikula

Maumivu ya daivetikula huwa ya kuchoma kama kisu na kunyonga, tatizo linaokuwa kubwa, maumivu huweza kudumu kwa muda wa siku kadhaa na mara nyingi hutokea upande wa kushoto mwa tumbo, hata hivyo inaweza kutokea pia upande wa kulia kwa nadra, na inapotokea upande wa kulia, maumivu huwa makali zaidi. Dalili zingine ni pamoja na homa au kutetemeka, kichefuchefu na kutapika, haja ngumu ay kuharisha.


Maumivu ya Henia

Huleta maumivu ya wastani, ya kuchoma au kuhisi mgandamizo kwenye eneo lenye henia. Maumivu huongezeka zaidi wakati mtu ana nyanyua vitu, kukimbia na shughuli zingine zinazoongeza shinikizo ndani ya tumbo. Baadhi ya watu uvimbe unaweza kutokea katika maeneo ambayo kuna henia, na pia dalili zingine za utumbo kufunga zinaweza kutokea.


Soma zaidi kuhusu henia katika makala ya 'Henia'


Mawe kwenye viungo ndani ya tumbo

Mawe haya hutokana na kuganda kwa madini ya kalisiamu inayopatikana kwenye maji ya tumbo au kwenye mkojo. Mawe hufanyika kwenye tumbo au kwenye viungo vingine kama figo, kibofu nyongo, kibofu cha mkojo, kongosho n.k. Mawe haya mbali na kuziba njia au mirija ya ogani za mwili, hupelekea maumivu makali ya tumbo wakati wa kutembea au kula au kukojoa. Kuna dalili zingine mbalimbali zinaweza kutokea ikitegemea na sehemu ya kiungo cha mwili kilichoathirika na mawe.


Soma zaidi kuhusu dalili, visababishi na matibabu ya mawe kwenye figo, kongosho na kibofu nyongo katika makala zingine ndani ya tovuti ya ULY CLINIC.


Matatizo ya mfumo wa uzazi

Kujisokota kwa korodani

Maumivu ya kujiviringa kwa korodani huwa na sifa ya kuanzia kwenye korodani kisha kuelekea tumboni upande mmoja wa korodani, dalili zingine zinazoweza kutokea ni kuvimba kwa korodani n.k. Kujiviringa kwa korodani ni dalili ambayo itahitaji uchunguzi na matibabu ya dharura ili kunusuru korodani.



Kujisokota kwa ovari

Kujiviringa kwa ovari husababisha kukata mawasiliano ya damu inayoenda kwenye ovari na hivyo hupelekea maumivu makali ya tumbo. Kujiviringa kwa ovari isipotibiwa mapema huweza pelekea kupasuka kwa ovari na maumivu makali sana ya tumbo. Kujiviringa kwa ovari huhitaji matibabu ya dharura ili kunusuru ovari.


Ujauzito nje ya kizazi

Ujauzito uliotungwa nje ya kizazi hupelekea maumivu makali ya tumbo, yanaweza kuanza kidogo na kuongezeka ukali. Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni kutokwa na damu ukeni.


Visababishi vingine

Visababishi vingine vya vichomi tumboni ni;


  • Sumu ya chakula- Hutokana na kula chakula ambacho kimeshashambuliwa na bakteria, mfano chakula kilicholala au kilichoota fangasi.

  • Kutostahimili laktosi- Hutokea kwa watu ambao hawana vimeng'enya vya kumeng'enya laktosi ambayo ipo kwenye maziwa.


Kuvimbiwa

Maambukizi ya UTI- Mbali na maumivu makali, maumivu hayo huweza kutokea wakati wa kukojoa na pia yanaweza kuelekea juu ya kibofu upande mmoja wa tumbo. Dalili zingine zinaweza kuwa kutokwa na mkojo mchafu au unaonuka


  • Sindromu ya iritabo bawel

  • Vidonda vya tumbo

  • Maumivu ya hedhi

  • Uchungu wa uongo


Soma maelezo zaidi kuhusu visababishi vingine vilivyoorodheshwa hapa katika makala zingine za ULY CLINIC.


Ufanye nini unapopata maumivu ya tumbo


Visababishi vingi vya maumivu makali ya tumbo(vichomi) huwa vinahitaji matibabu ya dharura, endapo unapata maumivu makali ya tumbo yanayodumu, tafuta huduma za dharura karibu nawe.


Dalili gani zinatakiwa kukufanya utafute matibabu ya dharura?


Endapo una dalili zifuatazo, fika hospitali mara moja au wasilaina na watoa huduma za dharura;


  • Kuishiwa pumzi

  • Homa

  • Kushuka kwa shinikizo la damu

  • Kutokwa na damu nyingi

  • Maumivu makali ya tumbo yanayodumu muda mrefu

  • Kuzimia


Wapi unapata taarifa zingine zaidi kuhusu kichomi tumboni?


Kusoma zaidi kuhusu kichomi, ingia kwenye makala nyingine za 'maumivu ya tumbo' au kwa kutafuta visababishi vilivyoandikwa mwanzoni mwa makala hii

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021, 04:53:42

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Patterson JW, et al. Acute Abdomen.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK459328/. Imechukuliwa 12.06.2021

2. UpToDate. Patient Education: Chronic Abdominal Pain in Children and Adolescents (Beyond the Basics). https://www.uptodate.com/contents/chronic-abdominal-pain-in-children-and-adolescents-beyond-the-basics?search=abdominal%20pain&source=search_result&selectedTitle=1~104&usage_type=default&display_rank=1. Imechukuliwa 12.06.2021

3. Cedars-Sinai. Abdominal Pain - Unexplained. https://www.cedars-sinai.org/health-library/diseases-and-conditions/a/abdominal-pain---unexplained.html. Imechukuliwa 12.06.2021

4. Macaluso CR, et al. Evaluation and Management of Acute Abdominal Pain in the Emergency Department. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3468117/. Imechukuliwa 12.06.2021

5. Appendicitis. hopkinsmedicine.org/health/conditions-and-diseases/appendicitis. Imechukuliwa 12.06.2021

6. Gallstones: Overview. my.clevelandclinic.org/health/diseases/7313-gallstones. Imechukuliwa 12.06.2021

7. Mayo Clinic Staff. (2019). Abdominal pain. mayoclinic.org/symptoms/abdominal-pain/basics/definition/sym-20050728. Imechukuliwa 12.06.2021

8. Symptoms and causes of indigestion.niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/indigestion-dyspepsia/symptoms-causes. Imechukuliwa 12.06.2021

9. Ovarian cysts. medlineplus.gov/ovariancysts.html. Imechukuliwa 12.06.2021

10. Stomach and abdominal pain.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/stomach-ache-and-abdominal-pain. Imechukuliwa 12.06.2021

11. UTI in adults: Symptoms and causes. niddk.nih.gov/health-information/urologic-diseases/bladder-infection-uti-in-adults/symptoms-causes. Imechukuliwa 12.06.2021

12. Viral gastroenteritis. niddk.nih.gov/health-information/digestive-diseases/viral-gastroenteritis. Imechukuliwa 12.06.2021

13. What Does a Diverticulitis Attack Feel Like? Symptoms & Risk Factors. https://www.healthline.com/health/digestive-health/what-does-a-diverticulitis-attack-feel-like. Imechukuliwa 12.06.2021

bottom of page