Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
3 Juni 2020, 08:51:19
Vidonda mdomoni
Vidonda mdomoni au vidonda ndani ya mdomo (kinywa) hujulikana kwa majina tofauti kama kanka, au apthous ulcer. Vidonda hivi huwa ni majeraha yaliyo na kina kifupi yanayoota kwenye sehemu laini ndani ya midomo chini ya fizi au chini ya ulimi. Bonyeza picha kuangalia zaidi.
Sifa za vidonda mdomoni
Vidonda hivi huwa na sifa zingine zifuatazo;
Huweza kutokea kimoja au zaidi ya kimoja
Haviambukizwi kama vilivyo vidonda vya homa baridi
Havitokei nje ya midomo, wala kwenye kona za midomo kama vilivyo vidonda vingine
Hupona ndani ya siku 7 hadi 10.
Dalili
Vidonda huwa na umbo la mduara na rangi nyeupe au njano katikati ya kidonda, kingo za kidonda huwa na rangi nyekundu. Vidonda hivi hufanyika ndani ya midomo, kwenye mashavu, fizi, au kwenye paa laini la kinywa.
Baadhi ya wagonjwa huwa na dalili za kuungua au kuchomachoma kabla ya kidonda kutokea
Vidonda vinaweza kuwa vidogo au vikubwa, vidonda vidogo hutokea sana na hupona ndani ya wiki mbili pasipo kuleta makovu wakati vidonda vikubwa huchelewa kupotea na huweza leta makovu ndani ya mdomo.
Visababishi
Visababishi vya vidonda mdomoni badi havifahamiki kimaanani, hata hivyo tafiti zimeonyesha kuwa kuna miunganiko ya mambo yanayopelekea kutokea kwa vidonda hivi kwa mtu.
Mambo yanayoweza kuamsha vidonda mdomoni ni pamoja na;
Mabadiliko ya homoni wakati wa hedhi kwa wanawake
Maambukizi ya H.pyrol anayesababisha vidonda vya tumbo
Msongo wa mawazo
Mzio na chakula au bakteria ndani ya kinywa mfano chocolate, kahawa, matunda forosadi, mayai, karanga, maziwa mtindi na vyakula vyenye viungo kwa wingi au pilipili
Kula chakula kinachokosa vitamin B12, madini ya zinc foleti na madini chuma
Majeraha kidogo kinywani kutokana na kupiga mswaki, kujing’ata, kutumia grili ya meno
Matumizi ya dawa na vimiminika vya kusafisha meno vyenye madini ya sodium sulfate
Magonjwa aina Fulani kama ugonjwa wa seliak, inflamatori baweli, bahcet, autoimmune, UKIMWI.
Vihatarishi
Kila mtu anaweza kupata vidonda mdomoni uwe na umri mkubwa au mdogo endapo, hata hivyo vidonda hivi hutokea sana kwa wanawake.
Watu wenye vidonda vinavyojirudia rudia mara nyingi huwa na historia kwenye familia ya vidonda hivi kwa sababu ya kurithi vinasaba au kuishi mazingira mamoja yenye vikereketa kama vile chakula n.k
Kinga
Kula mlo kamili
Kula vyakula kutoka kwenye makundi matano ya chakula ili kupata virutubisho vyote na kujikinga kupata vidonda hivi
Safisha kinywa vema kila siku
Safisha kinywa kila unapomaliza kula chakula na kusukutua mdomo mara moja kwa siku. Hakikisha kinywa chako hakina mabaki ya chakula ambayo yanaweza kuamsha vidonda. Tumia mswaki laini ili kuepuka kujeruhi kinywa chako wakati wa kupiga mswaki. Mswaki ulioharibika haufai kwa matumizi, usitumie nguvu kubwa kusafisha kinywa ili kuepuka majeraha.
Linda kinywa chako
Kama unatumia vifaa tiba mdomoni hakikisha kama kuna ncha zilizochomoza zimefunikwa ili kuepusha kupata majeraja.
Chunga kinachoingia mdomoni mwako
Jaribu kujizuia kula vyakula vinavyokereketa kinywa chako. Vyakula hivi ni kama vile karanga, chipsi, viungo aina Fulani, vyakula vyenye tindikali, kama nanasi, zabibu, forosadi, machungwa na ndimu. Usitumie chakula ambacho kina kuletea mzio.
Punguza msongo wa mawazo
Endapo vidonda vyako vinatokana na msongo wa mawazo, tumia mbinu za kupunguza msongo huomfano kwa kuwa na kipindi cha kujitafakari kwa meditation.
Wakati gani uonane na daktari?
Ongea na daktari wako endapo unapata vidonda hivi mara kwa mara na vyenye maumivu makali na dalili zilizoorodheshwa hapa chini;
Vidonda vinavyokua kuelekea kwenye midomo
Endapo unapaya maumivu makali ya kinywa usiyoweza kuvumilia
Kushindwa kula au kunywa
Homa kali inayoambatana na vidonda
Vidonda vikubwa mdomoni
Vidonda vinavyojirudia rudia, endapo kidonda kipya kinatokea kabla ya cha zamani kutoweka au kutokea kwa mlipuko wa mara kwa mara
Vidonda vinavyodumu zaidi ya wiki mbili
Matibabu
Vidonda vya apthous huwa havina tiba. Matibabu yaliyopo hulenga;
Kupunguza dalili unazopata za kuhisi maumivu makali
Kukuwezesha uweze kula chakula na kusafisha kinywa pasipo kupata maumivu
Kupunguza uvimbe kwenye kidonda ili kufanya kidonda kipone haraka
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
8 Oktoba 2021, 04:53:44
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.Canker sores. American Academy of Oral Medicine. http://www.aaom.com/index.php?option=com_content&view=article&id=82:canker-sores&catid=22:patient-condition-information&Itemid=120. Imechukuliwa 3.6.2020
2.Canker sores. American Dental Association. https://www.mouthhealthy.org/en/az-topics/c/canker-sores. Imechukuliwa 3.6.2020
3.Canker sores. FamilyDoctor.org. http://familydoctor.org/familydoctor/en/diseases-conditions/canker-sores.html. Imechukuliwa 3.6.2020
4.Recurrent aphthous stomatitis. The Merck Manual Home Edition. http://www.merckmanuals.com/home/mouth_and_dental_disorders/symptoms_of_oral_and_dental_disorders/recurrent_aphthous_stomatitis.html. Imechukuliwa 3.6.2020
5.Recurrent aphthous ulcerations. American Academy of Oral and Maxillofacial Pathology. http://www.aaomp.org/public/aphthous-ulcerations.php. Imechukuliwa 3.6.2020
6.Mouth sores and inflammation. The Merck Manual Home Edition. http://www.merckmanuals.com/home/mouth_and_dental_disorders/symptoms_of_oral_and_dental_disorders/mouth_sores_and_inflammation.html. Imechukuliwa 3.6.2020