top of page

Dalili na viashiria vya magonjwa mbalimbali

ULY Clinic inakushauri kufuata ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala. Bofya picha au neno soma zaidi ili kuingia kwenye makala kwa undani.

Chuchu kuuma

Chuchu kuuma

Maumivu ya chuchu yanayosababishwa na unyonyeshaji mbaya, maambukizi, au msuguano, yanaweza kutibiwa kwa dawa, tiba za nyumbani, na utunzaji sahihi wa ngozi. Ikiwa maumivu yanaendelea au yanazidi kuwa makali, ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi zaidi.

Mkojo wenye povu

Mkojo wenye povu

Ni hali inayoweza kutokea kwa mtu yeyote ambayo mara nyingi husabaishwa na sababu zisizo magonjwa na wakati mwingine zinaweza kuhusiana na magonjwa.

Matege ya magoti kugusana

Matege ya magoti kugusana

Ni hali ya kawaida kwa watoto na mara nyingi hujirekebisha yenyewe bila matibabu. Hata hivyo, ni muhimu kutambua hali zinazoweza kusababisha genu valgum ya kipatholojia ili kuhakikisha uchunguzi na matibabu sahihi.

Miguu upinde

Miguu upinde

Ni hali ambapo miguu inajikunja kuelekea nje kwenye magoti, na kusababisha nyayo na vifundo vya miguu kugusana huku magoti yakiachana mbali. Hali hii inayosababishwa na matatizo kadhaa huwa na matibabu mbalimbali.

Maumivu ya kitovu kwa mtoto

Maumivu ya kitovu kwa mtoto

Zipo sababu nyingi za maumivu ya kitovu kwa mtoto kutoka matatizo madogo kama gesi hadi magonjwa makubwa yanayohitaji matibabu ya haraka. Ni muhimu kuwa makini na dalili zinazoambatana na maumivu haya na kumpeleka mtoto kwa daktari haraka ikiwa hali inazidi kuwa mbaya.

bottom of page