Mwandishi: ULYCLINIC
​
18.07.2018
​
Jinsi gani unaweza kugundua kwamba una ujauzito?
Hili ni jambo la msingi linalotakiwa kufanyika wakati wa mahudhurio ya klinic ya wajawazito
Kugunduliwa kwa ujauzito kunategemea mambo mawili
-
Dalili anazopata mama na kupelekea kusema kwamba ana ujauzito na
-
Dalili zinazoonekana na kupelekea kusema mama anam ujauzito
Dalili zifuatazo zinaweza kutokea kwa mama mwenye na kuonyesha kwamba ana ujauzito;
Kutoingia hedhi. Mara nyingi huwa dalili ya kwanza kabisa kwamba kunaujauzito. Iangaliwe kwa umakini pia kwamba kutoona hedhi kwa mwanamke kunaweza kusababishwa na mambo mengine kama vile, kutotolewa kwa yai, msongo wa mawazo ama kazi nzito,magonjwa sugu, ama kunyonyesha
Dalili zingine anazoweza kupata mwanamke mjamzito kutegemea mtu na mtu ni kama
-
Matiti kujaa na kuuma yakishikwa
-
Mabadiliko katika ngozi
-
kichefuchefu,
-
Kutapika,
-
Kukojoa mara kwa mara,
-
Kuchoka mwili,
Kati ya wiki ya 12 na 20 mama mjamzito ataona tumbo likiwa linakuwa na kuhisi mtoto akicheza tumboni
Kipimo cha ujauzito kwa njia ya mkojo (kugundua homoni ya B-HCG)
Ni kipimo kinachotumika sana na huwa cha uhakika zaidi, huweza kutambua ujauzito kuanzia wiki moja baada ya kujipandikiza kwa mtoto ndani ya mfuko wa kizazi cha mama ama siku chache baada ya kukosa kuona hedhi (siku 14 toka katikati ya mzunguko wa hedhi)
Mkojo wa kwanza wa asubuhi ni mzuri na mapema ni mzuri kutumika kupima ujauzito kwa sababu huwa na kiwango
Kipimo cha damu (kugundua homoni ya B-HCG)
Kipimo hiki kinaweza kugundua ujauzito mapema zaidi ya kile cha mkojo,kiwango cha B-HCG hufikia kiwango cha juu zaidi siku kuanzia ya 60 ama 70 ya ujauzito na kasha huanza kushuka
Kipimo hiki kwa hivyo ni kizuri kwa kutofautisha kama ujauzito ni wa kawaida ama ni ujauzito usio wa kawaida uitwao molar pregnancy
Mapigo ya moyo ya mtoto
Huanza kusikika mapema zaidi kati ya wiki ya 9 hadi 10 kutoka siku ya mwisho kuona siku kwa mwanamke kwa kutumia kipimo cha umeme cha Doppler.
Kwa kutumia kipimo cha fetoscope ambacho mara nyingi hufanywa na clinic huweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto kuanzia wiki ya 18 hadi 20 kutoka siku ya mwisho ya kuona hedhi
Mtoto kucheza tumboni
Mama anaweza kusikia kwa mara ya kwanza kuanzia wiki ya 16 hadi 18 na huonyesha kuwa mtoto yupo hai.
​
​
Imeboreshwa 09/08/2021
​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​
-
Huduma za kliniki wakati wa ujauzito
-
Namna ya Kujua tarehe ya kujifungua