Kutokwa na damu ukeni baada ya hedhi kukoma
Imeandikwa namadaktari wa uly clinic
Komahedhi ni ishara au neno limalomaanisha hedhi kuisha, maelezo ya kitaalamu humaanisha pale mwanamke anapoacha kuona damu ya mwezi kwa miezi 12 mfululizo.
Kutokwa damu baada ya hedhi kukoma hua sio jambo la kawaida na inapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu endapo mwanamke amepata hali hii.
Kwa mafano, kutokwa damu ukeni baada ya komahedhi kunaweza kusababishwa na matatizo kama haya yalioorodheshwa hapo chini;
-
Saratani ya mfuko wa kizazi, ikiwa pamoja na saratani ya kuta za ndani ya kizazi, saratani ya misuli ya kizazi, saratani ya shingo ya kizazi
-
Kusia kwa kuta za uke au kusinya kwa kuta za ndani ya kizazi.
-
Fibroid ndani ya kizazi
-
Vinyama ndani ya kuta za uzazi
-
Maambukizi ndani ya mfuko wa kizazi
-
Matumizi ya madawa kama homoni au dawa inayoitwa tamoxifen
-
Majeraha kwenye uzazi
-
Kutokwa damu kutoka kwenye mfumo wa mkojo, au njia ya haja kubwa
-
Kukua kupitiliza kwa seli ndani ya mfuko wa kizazi
Sababu zinazosababisha kutokwa na damu baada ya komahedhi zinaweza kuwa si za kudhuru, ingawa kuona damu baada ya komahedhi kunaweza kusabaishwa na tatizo kubwa ndani ya mwili, hivyo ni muhimu kuonana na daktari ili kupata uchunguzi na matibabu sahihi.
Imeandikwa 3/5/2018
Imenoreshwa 3/11/2018