Imeandikwa na Daktari wa ULY-clinic
Kutokwa na damu
Kutokwa na damu muda mrefu huweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ikiwa pamoja na majeraha ya upasuaji mkubwa na matumizi ya dawa za kuyeyusha damu.
Visababishi vingine huwa pamoja na;
Magonjwa ya kutokwa damu yanayosababishwa na;
-
Madhaifu kwenye chembe sahani za damu(pletileti)
-
Ugonjwa wa hemofilia
-
Shinikizo la damu la juu lisilodhibitiwa
-
Matumizi ya dawa jamii NSAID’s kama aspirini ambazo huingiliana na kazi za chembe za damu za pletilet
-
Upungufu wa vigandisha damu
-
Magonjwa ya ini
-
Kunywa dozi kubwa kupita kiasi ya dawa kuyeyusha damu
-
Upungufu wa Vitamini K
-
Matumizi ya dawa za kuyeyusha damu mfano warfarin, heparin, n.k
Dalili
Dalili za kutokwa na damu zinaweza kuwa pamoja na;
-
Kutokwa na damu kwenye mkojo au kinyesi
-
Kuumia kirahisi na kutokwa sana na damu mara baada ya kuumia
-
Kuchoka sana
-
Kupata majeraha ambayo hayakatiki damu
-
Maumivu ya maungio kutokana na kutokwa na damu ndani ya maungio
-
Kutokwa na damu puani bila kuwa na sababu ya msingi
-
Maumivu makali ya kichwa amabayo hayaishi
-
Kutokwa na damu muda mrefu kuliko mtu mwingine akijikata, kungolewa jino na kufanyiwa upasuaji
-
Maumivu ya ghafla, kuvimba na kuhisi joto kwenye maungio ya magoti
-
Kutoona vema, kama vile kuona vitu viwiliviwili
-
Kutapika kunakojirudia
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii
Imepitiwa 12.06.2020
Rejea
-
ULY clinic
-
Riley Childrens’s Health, Coagulation disorder kwenye linki ya https://www.rileychildrens.org/health-info/coagulation-disorders. Imechukuliwa 11.06.2020
-
Bleeding. (n.d.).stjohn.org.nz/First-Aid/First-Aid-Library/Bleeding. Imechukuliwa 12.06.2020
-
Clinical transfusion practice: Guidelines for medical interns. (n.d.).who.int/bloodsafety/transfusion_services/ClinicalTransfusionPracticeGuidelinesforMedicalInternsBangladesh.pdf. Imechukuliwa 12.06.2020
-
Mayo Clinic Staff. (2017). Severe bleeding: First aid. mayoclinic.org/first-aid/first-aid-severe-bleeding/basics/art-20056661. Imechukuliwa 12.06.2020
-
Learn first aid for someone who is bleeding heavily. (n.d.).redcross.org.uk/first-aid/learn-first-aid/bleeding-heavily. Imechukuliwa 12.06.2020
-
Stop the bleed. (2018).dhs.gov/stopthebleed. Imechukuliwa 12.06.2020