Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
Kutokwa na damu kwenye kinyesi
Tatizo la damu kwenye kinyesi huweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali ikiwepo Bawasili, Kuhara, saratani ya utumbo mpana na matatizo mengine kama yalivyoorodheshwa kwenye visababishi.
Mtu anaweza kuwa na damu inayoonekana nyekundu, nyeusi, au nyekundu iliyoganda. Lakini pia mtu anaweza kutoa mabonge ya damu wakati wa kujisaidia bila kutoa kinyesi. Dalili hizi mbalimbali husababishwa na sababu aina tofauti tofauti
Kutokwa na damu nyeusi wakati wa kujisaidia kunaweza kumaanisha damu imevuja mfumo wa juu wa tumbo kuanzia kwenye maeneo ya mrija wa esofagasi, tumbo la chakula, utumbo mwembamba na sehemu ya utumbo mpana. Hata hivyo endapo mtu anatoka kiasi kukubwa cha damu kwenye maeneo haya damu nyekundu inaweza kuonekana kwenye kinyesi ikiwa pamoja na mchanganyiko w akinyesi cheusi.
Kutokwa na damu nyekundu kama inavyotokea kwa mtu aliyejikata na kitu, humaanisha damu inavuja kwenye maeneo ya utumbo mpana na rektamu(kifuko cha kutunzia kinyesi) au sehemu ya nje kabisa ya tundu la kupitisha kinyesi.
Ni ni visababishi?
Bawasili- huongoza kusababisha tatizo la kutokwa na damu kwenye kinyesi, damu huonekana kuwa nyekundu, inaweza kutoka mwanzoni pamoja na haja kubwa, kutoka kama michirizi ya damu kwenye kinyesi au kutoka mwishoni mwa kinyesi. Dalili zingine zinaweza ambatana na tatizo hili la bawasili. Bonyeza kusoma Zaidi kuhusu bawasili kwenye Makala ndani ya tovuti hii.
Ugonjwa wa Diverticular.-Diverticula ni vijifuko vidogo vinavyochomoza katika utumbo mpana. Kwa kawaida havina shida yoyote, hata hivyo baadhi ya nyakati huweza kutoa damu au kupata maambukizi yanayoambatana na kuonyesha dalili ya maumivu ya tumbo.
Mipasuko njia ya haja kubwa- hii ni mipasuko midogo kama inayotokea kwenye midomo. Mipasuko hii husababishwa na kupitisha kinyesi kikubwa kilicho kigumu kwenye tundu la kutolea haja kubwa.
Ugonjwa wa colitis- husababihswa michomo inayotokana na maambukizi kwenye utumbo mpana. Kisababishi kikubwa huwa ni ugonjwa wa infamatori bawel
Angiodysplasia. Hii husababishwa na madhaifu ya mishipa ya damu kwenye njia za mfumo wa chakula, mishipa hii hupasuka kirahisi na kutoa damu.
Vidonda vya tumbo- vidonda ndani ya tumbo na utumbo huweza kuvuja na kutoa damu. Mara nyingi damu ya vidonda vya tumbo hutoka nje ya mwili kwa ishara ya kuw ana kniyesi kinachonata kama gundi na cheusi. Vidonda vya tumbo huweza kusababishwa na maambukizi ya bakteria anayeitwa H.pyrol au uzalishwaji wa tindikali kwa wingi. Matumizi ya muda mrefu ya dawa jamii ya NSAIDs kama aspirini, ibuprofen, na naproxen.
Polipsi njia ya haja kubwa- ni vijivimbe ambavyo vinachomoza ndani ya utumbo, vivimbe ivi vinaweza kupasuka na kutoa damu. Polipsi baadhi ya nyakati zinaweza kubadilika kuwa saratani.
Saratani- Kuna saratani mbalimbali zinazoweza kusababisha damu kwenye kinyesi kama vile saratani ya kolorekto- saratani hii husababisha damu kwenye kinyesi ambayo hainekani kwa macho ya kawaida.
Magonjwa ya mrija wa esophagus- kuchanika kwa mrija, au kuvimba kwa mishipa ya damu kwenye mirija hii kutokana na sababu mbalimbali inawez akupelekea mtu kupata damu kwenye kinyesi.
Daktari atakuchunguza kwenye maeneo haya na kukuuliza maswali mbalimbali ili kujua visababishi, pia utapimwa baadhi ya vipimo kulingana na kisababishi ambacho daktari amekiona. Baadhi ya visababishi ata hivyo havihitaji vipimo.
Soma pia kuhusu rangi ya kinyesi na maana yake kitaalamu kwa kubonyeza hapa
ULY CLINIC inakushauri sikuzote utafute msaada kutoka kwa daktari wako mwenye weledi, anayetambulika na aliyesajiliwa na MCT mara utakapoona kuwa na dalili zinazoendana na makala hii kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ili upate tiba kulinganana tatizo lako halisi.
ULY CLINIC pia inakushauri kwa urahisi wa kupata na kusoma makala zetu, weka app kwenye simu yako kwa kubonyeza hapa
Imeboreshwa, 4.12.2020
Rejea za mada hii
-
MedlinePlus: "Bloody or tarry stools." Nebraska Colon Cancer Screening Program: "Rectal Bleeding: What You Should Know."
-
Zitelli BJ, et al., eds. Zitelli and Davis' Atlas of Pediatric Physical Diagnosis. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 4.12.2020
-
Walls RM, et al., eds. Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 9th ed. https://www.clinicalkey.com.Imechukuliwa 4.12.2020
-
MedlinePlus: "Gastrointestinal fistula."
-
NYU Langone Medical Center: "Angiodysplasia of the Colon."
-
National Digestive Diseases Information Clearinghouse: "Bleeding in the Digestive Tract."
-
The Ohio State University Medical Center: "Peptic Ulcers."
-
WebMD. https://www.webmd.com/digestive-disorders/blood-in-stool#3.Imechukuliwa 4.12.2020
-
Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional. Imechukuliwa 4.12.2020
-
Kliegman RM, et al. Nelson Textbook of Pediatrics. 20th ed. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 4.12.2020