Imeandaliwa na daktari wa ULY-Clinic
​
Damu kwenye mbegu za kiume-Shahawa
​
Mwanaume anapomwaga shahawa wakati wa kujamiana, shahawa hizo huwa na mchanganyiko wa majimaji yaliyotolewa katika tezi mbalimbali kwenye mfumo wa uzazi kama teze dume, n.k. Shahawa na majimaji hupita katika mirija mbalimbali hadi kufika nje ya mwili kupitia mrija unatoa mkojo nje ya mwili (yurethra), njia hizi huwa na mishipa ya damu na hivyo endapo kuna tatizo katika mirija hiyo kama maambukizi au matatizo mengine mbalimbali, hupelekea kuvilia damu ndani ya mirija na kuonekana kama mchanganyiko wa damu kwenye shahawa au mkojo.
​
Dalili
​
Dalili ya kutokwa na damu kwenye mbegu za kiume huonekana pale mtu anapofika kileleni ambapo humwaga;
​
-
Shahawa zilizo na rangi nyekundu au
-
Shahawa zilizochanganyika na matone ya damu
​
​
Dalili za hatari zinazohitaji uchunguzi ni
Ukiwa na dalili zifuatazo, pata uchunguzi wa haraka
​
-
Kuhisi uvimbe kwenye njia ya haja kubwa
-
Kuishi kwenye maeneo ambayo kuna maambukizi mamkubwa ya kichocho (saas hivi au muda uliopita)
-
Kutokwa na damu zaidi ya mwezi mmoja ( isipokuwa endapo umefanyiwa upasuaji wa kukata nyama kwenye tezi dume)
-
Tatizo kujirudia rudia
-
Una umri zaidi ya miaka 35
-
Una historia ya saratani
-
Una madhaifu ya mfumo wa mkojo
-
Umekuwa kwenye kihatarishi cha kupata magonjwa ya zinaa (kwa kuwa na wapenzi wengi pia kutotumia kondomu)
-
Kupata homa, kupoteza uzito bila sababu na kutokwa jasho wakati wa usiku.
​
Visababishi
​
Visababishi vya kuonekana kwa damu kwenye mbegu za kiume huwa hazijulika sana.
​
Kwa wanaume walio na umri chini ya miaka 40 maambukizi ni kisababishi kikubwa, maambukizi haya huambatana na dalili zingine kama homa, kutetemeka, maumivu ya maeneo ya siri, ugumu wa kukojoa na damu kwenye mkojo .
Kwa wanaume walio zaidi miaka 40, damu kwenye mbengu huashiria saratani na mara nyingi ni saratani ya tezi dume, hivyo uchunguzi makini unahitajika kwa watu walio kwenye kundi la umri huu hata hivyo hatari ya kupata saratani huwa ni ndogo sana.
Tafiti zinaonyesha kuwa, zaidi ya wanaume 800 waliokuwa na tatizo la damu kwenye mbegu za kiume, saratani ilikuwa ni moja ya kisababishi lakini mchango wake ulikuwa chini ya asilimia 4 ya visababishi.
​​
Sababu zaidi zinazosababisha damu kweye shahawa
-
Maambukizi ya chlamidia
-
Maambukizi kwenye mirija ya epidydimis (Epidymitis)
-
Kukatisha ghafla tendo la kujamiana wakati wa kujamiiana
-
Kuacha kufanya ngono kwa muda mrefu
-
Kukatwa kinyama kwenye tezi dume kwa ajili ya vipimo
-
Matatizo ya mfumo wa mkojo mfano, vinyama kwenye kibofu, mrija wa urethra au tezi dume
-
Kufanyiwa upasuaji wa kutoa tezi dume
-
Kuwa na mishipa dhaifu ya damu
-
Ugonjwa wa kurithi wa hemophilia
-
Saratani ya korodani
-
Upungufu wa chembe sahani za damu
-
TB ya mfumo wa mkojo
-
Ugonjwa wa von willbrand
Wakati gani wa kumwona daktari haraka?
Endapo huna dalili za hatari hauna sababu ya kumwona daktari haraka, hata hivyo utatakiwa kuonana na daktari ndani ya wiki mbili ili kupata ushauri na vipimo endapo vitashauriwa na daktari wako.
Endapo una umri chini ya umri wa miaka 35 haupaswi pia kumwona daktari isipokuwa endapo una dalili za hatari.
Endapo una umri zaidi ya miaka 35 hata kama huna dalili zingine za hatari unapaswa kuonana na daktari ndani ya wiki mbili kwa ushauri na vipimo.
​
Vipimo
Mara nyingi wanaume walio chini ya umri wa miaka 35 au 40 na wale waliofanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi dume, kutokwa na shahawa zilizochanganyika na damu hakutakiwi kukuogopesha sana kwani tatizo huwa linaisha lenyewe ukilipa muda.
Vipimo ambavyo huagizwa kufanyika kwa wanaume walio kwenye umri huu mara nyingi ni vile vya kutambua maambukizi ambavyo ni;
-
Kipimo cha urinalysis
-
Urine culture
Endapo daktari ataona kuna dalili za hatari kwako ataamua kukufanyia vipimo vingine ambavyo ni;
-
Kipimo cha biopsy kuangalia uwezekano wa saratani ya tezi dume kwa wanaume waliovuka umri wa miaka 40
-
Kipimo cha Prostate specific antigen (PSA)
-
Ultrosound aina ya TRUS
-
MRI
-
Cystoscopy
Matibabu ya damu kwenye mbegu za kiume
-
Matibabu ya tatizo hili hulenga kisababishi kilichofahamika.
​
​
Imeboreshwa, 09.06.2021
​
​
Rejea za mada hii
​
-
Anuja P. Shah MD, David Geffen School of Medicine at UCLA. Blood in Semen MSD professional manual. https://www.msdmanuals.com/home/kidney-and-urinary-tract-disorders/symptoms-of-kidney-and-urinary-tract-disorders/semen-blood-in. Imechukuliwa 2.1.2020
-
Weiss BD, et al. Hematospermia. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 2.1.2020
-
Merck Manual Professional Version. Hematospermia. https://www.merckmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/symptoms-of-genitourinary-disorders/hematospermia. Imechukuliwa 2.1.2020
-
Warfarin. Micromedex 2.0 Healthcare Series. http://www.micromedexsolutions.com. Imechukuliwa 2.1.2020