top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

 

Kutokwa na damu puani

 

Kutokwa na damu ndani ya pua kwa lugha tiba huitwa epistaksizi, huweza kutokea kipindi cha ujana au utotoni kwenye umri fulani. Tatizo hili husababisha hofu kwa mzazi au mtoto, hata hivyo huna haja ya kuogopa kwa sababu tatizo hili mara nyingi huwa si hatari na karibia kila mtu ashapata mara moja katika maisha yake. Hata hivyo endapo unatokwa na damu puani zaidi ya mara moja kwa wiki unatakiwa kupata uchunguzi kutoka kwa daktari.

 

Kuta za pua zimetengenezwa na mishipa ya damu midogomidogo iliyo karibu na ngozi ya pua kwa ndani, kuta hizi zinapopata hewa kavu au kubanwa wakati wa kupeng’a mafua, mishipa ya damu hupasuka hivyo kusababisha mtu kutokwa na damu.

 

Visababishi

 

Visababishi vingine huwa pamoja na;

 

  • Maambukizi kwenye sainazi

  • Mzio

  • Matumizi ya aspirini

  • Magonjwa ya kutokwa na damu kama hemophilia

  • Matumizi ya dawa za kuyeyusha damu kama aspirini, warfarin, heparin, Dabigatran, Rivaroxiban, Apixaban, Edoxaban, Fondaparinux na Clopidogrel

  • Sumu na kemikali kama ammonia

  • Maambukizi sugu kwenye sainazi

  • Matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeini

  • Homa baridi

  • Kuhama kwa ukuta wa kati wa pua

  • Kuingiliwa na kitu kigeni puani

  • Kutumia dawa za kupuliza puani

  • Rinaitizi isiyosababishwa na mzio

  • Kupigwa/ kujiumiza puani

  • Matumizi ya pombe

  • Magonjwa ya kurithi ya kutokwa na damu

  • Saratani ya damu

  • Saratani kwenye pua

  • Polipsi puani

  • Ujauzito

  • Kufanyiwa upasuaji wa pua

 

Wakati gani wa kumwona daktari?

 

Endapo unapata dalili zifuatazo tafuta msaada kutoka kwa daktari haraka;

 

  • Kutokwa na damu nyingi sana au kushindwa kupumua kwa sababu ya damu kutoka

  • Mtoto anabadilika rangi kwenye macho, kupauka viganja vya mikono au ulimi, kuchok u kupoteza fahamu

  • Damu haikati licha ya kufanya mbinu zote za matibabu nyumbani kama zilivyoorodheshwa hapa chini

  • Una historia ya kufanyiwa upasuaji puani hivi karibuni au una saratani ya pua

  • Umepata ajali puani inayosababisha damu kutoka, mfano kugonjwa usoni na endapo unahisi kwamba una majeraha Zaidi ya kutokwa na damu (kuvunjika mifupa ya sakafu ya fuvu)

  • Imeambatana na dalili zingine za maumivu ya kifua

  • Damu inatoka na unatumia dawa za kuyeyusha damu kama vile warfarin, heparin, clopidrogrel n.k

  • Kama damu inajirudia kutoka mara kwa mara na una bruizi sehemu zingine za mwili

​

Matibabu

 

Matibabu dawa huhusisha

 

  • Dawa za maumivu na kupaki pua kwa kutumia gozi yenye dawa- kumbuka unatakiwa kuwa makini kwa sababu mgonjwa anaweza kukosa hewa.

  • Matibabu ya dawa za kuzuia maambukizi na sindromu shoku ya sumu kutokana na maambukizi

  • Kuzuia kutumia dawa jamii ya NSAIDS kama aspirin, ibuprofen na zinginezo

 

Namna ya kujitibu mwenyewe

 

  • Peng’a pua ili kuondoa damu iliyoganda, fanya hivi taratibu hii inaweza kuongeza damu kutoka lakini usihofu. Kwa watoto wadogo kufanya hivi si lazima

  • Pinda mgongo kwa mbele ukiwa umekaa au kusimama. Usilalie mgongo kwa sababu inaweza kusababisha utapike

  • Bana pua karibu na matundu kwa kutumia vidole viwili vya mikono yako, tumia nguvu sawa kubana matundu yote kwa pamoja

  • Bana maka kuziba matundu ya pua kwa angalau dakika 5 kwa watoto au 10 hadi 15 kwa mtu mzima. Hakikisha unatumia saa kuhesabu muda huu, watu wengi huacha kubana chini ya muda unaoshauriwa hivyo damu huendelea kutoka.

  • Endapo unaweza tumia barafu kupaki kweye kuta za pua, hii inasaidia pia mishipa ya damu kusinyaa na kusimamisha damu kutoka lakini si lazima kufanya hivi

 

Endapo umefuata maelezo yaliyoorodheshw ahapo chini na damu bado inaedelea kutoka, rudia upya kwa muda wa dakika 30. Na endapo bado inaendelea kutoka, tafuta msaada kutoka kwa daktari wako haraka au piga simu kuita mtaalamu wa afya kuja kukusaidia.

 

Kujikinga na damu kutoka puani

 

  • Tumia humidifaya ili kuongeza unyevu kwenye mazingira yako endapo hewa ni kavu

  • Tumia dawa ya maji ya chumvi kupuliza puani ili kufanya pua iwe na unyevunyevu

  • Jizuie kuingiza kidole puani, kama ni lazima kata kucha zako ziwe fupi kuzuia kujiumiza.

 

​

Wasiliana na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba
​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.

 

 

Imeboreshw a mara ya mwisho, 12.06.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. Nosebleed patient education. https://www.uptodate.com/contents/nosebleeds-epistaxis-beyond-the-basics. Imechuliwa 12.06.2020

  2. Messner AH. Management of epistaxis in children. http://www.uptodate.com/home. Imechuliwa 12.06.2020

  3. Messner AH. Epidemiology and etiology of epistaxis in children. http://www.uptodate.com/home. Imechuliwa 12.06.2020

  4. Messner AH. Evaluation of epistaxis in children. http://www.uptodate.com/home. Imechuliwa 12.06.2020

  5. Ferri FF. Epistaxis. In: Ferri's Clinical Advisor 2015: 5 Books in 1. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2015. http://www.clinicalkey.com. Imechuliwa 12.06.2020

  6. Marx JA, et al. Otolaryngology. In: Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 8th ed. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2014. http://www.clinicalkey.com. Imechuliwa 12.06.2020

  7. Nosebleeds. American Academy of Otolaryngology — Head and Neck Surgery. http://www.entnet.org/content/nosebleeds. Imechuliwa 12.06.2020

bottom of page