Damu ukeni baada ya kujamiana(mwanamke)
Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Kutokwa damu baada ya kujamiana ni hali inayotokea sana na huweza kutokea hata usipokuwa kwenye siku zako au hutarajii kuona siku zako hivi karibuni. Kutokwa na damu ukeni huwa haimaaninishi kutokwa damu kwenye tundu la ukeni tu bali kutokwa na damu sehemu mbalimbali za maeneo ya siri kama kwenye tundu la mkojo, mashavu ya uke n.k
​
Kutokwa damu baada ya kujamiana hutokea sana kwa vijana wadogo, na wale wanaoelekea kipindi cha komahedhi na haimaanishi wakati wote kwamba kuna tatizo kubwa au unahitaji kuonana na daktari haraka. Lakini kutokwa na damu baada ya tendo la kujamiana kwa watu wenye umri mkubwa na walio kwenye kipindi cha komahedhi(postmenopousal), hutakiwa kupewa kipambele cha haraka cha kumwona daktari kwa sababu huwa si tatizo linalotokea sana. Pata uchunguzi kama unatokwa damu kipindi hiki
​
Endelea kusoma kuhusu visababishi kwa kubonyeza hapa
Wasiliana na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba
​
​
​
Imeboreshwa, 06.12. 2020
​
Rejea za mada hii
​​
-
Kaunitz AM etal. Differential diagnosis of genital tract bleeding in women. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 06.11.2019
-
Shapley M etal. Postcoital bleeding in women. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 06.11.2019
-
Frequently asked questions. Abnormal uterine bleeding. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Abnormal-Uterine-Bleeding. Imechukuliwa 06.12.2020