Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Mangwella S, MD

Ni dawa ya kuua bakteria yenye wigo mpana dhidi ya vimelea jamii ya gramu hasi na chanya. Huweza kutibu maambukizi katika sehemu mbalimbali kama ngozi, mfumo wa upumuaji, tishu laini, ubongo na mfumo wa mkojo.
Kundi la dawa
Ceftriaxone ni kizazi cha tatu cha dawa jamii ya cephalosporin.
Upekee wa ceftriaxone na dawa zingine kwenye kundi lake
Nusu maisha ya dawa ya ceftriaxone ni mkubwa ukilinganisha na dawa zilizo kwenye kundi moja.
Ceftriaxon pia huwa na uwezo mkubwa zaidi kuua bakteria jamii ya gramu hasi kuliko dawa za kizazi cha kwanza na cha pili cha cephalosporin.
Majina ya kibiashara
Ceftriaxone hufahamika kwa majina ya ibishara kama;
Rocephin
Pawercef
Aacef
Abxone
Accuzon
Acticef
Aerocef
Afzone
Alcef
Ceftrimax
Ceftivo
Gramocef
Infoxon T
Vimelea wanaouliwa na ceftriaxone
Vimelea wanaouliwa na ceftriaxone ni;
Streptococcus pneumoniae
Streptococcus pyogenes (Kundi A beta-hemolytic streptococci)
Coagulase-hasi staphylococci
Baadhi ya spishi wa Enterobacter spp
Haemophilus influenza
Neisseria gonorrhoeae
Proteus mirabilis
Eschelician coli
Spishi wa Klebsiella
M. catarrhalis
B. burgdorferi na
Baadhi ya vimelea jamii ya anaerobes
Ceftriaxone hutibu nini?
Ceftriaxone hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayotokana na maambukizi ya bakteria wanaodhuriwa na dawa hii miongoni mwayo ni;
Jipu kwenye ubongo
Maambukukizi ya bakteria kwenye moyo
Maambukizi ya bakteria kwenye sinus
Maambukizi ya bakteria kwenye mifupa
Chancroid
Nimonia ya jamii
Gono ya macho kwa vichanga
Kuvimba kwa korodani kutokana na maambukizi
Kuvimba kwa kidaka tonge kutokana na maambukizi
Gono kwenye maungo ya mwili
Maambukizi kwenye mfumo wa chini wa upumuaji
Gono ya ndai ya via vya uzazi
Maambukizi ndani ya tumbo
Taifodi
Kusambaa kwa bakteria kwenye damu
Ugonjwa wa lyme
Homa ya uti wa mgongo kutokana na maambukizi ya bakteria
Kuzuia maambukizi kabla ya upasuaji
Kusambaa kwa bakteria kwenye maungo ya mwili
Shigelosis
Maambukizi tata ya bakteria kwenye mfumo wa mkojo
Kaswende
Gono ya kwenye uke
Ugonjwa wa whipple
Maambukizi ya bakteria kwenye mfumo wa kati wa sikio
Gono isiyo sugu
UTI isiyo sugu
Namna ceftriaxone inavyofanya kazi
Ceftriaxone hutumika kua bakteria na mara nyingi bakteria jamiii ya gramu chanya. Dawa hii pia huwa na uwezo kwenye bakteria jamii ya gramu hasi na anaerob. Uwezo wake wa kutibu hutokana na dawa hii kuzuia uzalishaji wa vijenzi muhimu vya uzio wan je wa bakteria vyenye jina la mucopeptide kwa kujishikiza kwneye vimeng’enya vya carboxypeptidases, endopeptidases na transpeptidases. Kujishikiza kwenye vimeng’enya hivi hufanya bakeria kushindwa zalisha uzio wake wa nje na hivyo kufa
Ufyonzwaji wa ceftriaxone
Hutolewa kwa kuchoma kwenye misuli au kuingia kwenye mishipa ya damu. Ufyonzwaji wake tumboni ni chini ya asilimia 1 na hii ndio maana dawa huwa haitolewi kwa kunywa.
Utoaji dawa mwilini
Asilimia 33 hadi 66 ya Ceftriaxone hutolewa mwilini kupitia mkojo, kiasi kilichobaki hutolewa kwenye damu kupitia haja kubwa.
Nusu maisha ya dawa
Nusu maisha ya dawa ceftriaxone ni masaa 5.8. hadi 8.7. nusu maisha kwenye majimaji yaliyo kwenye mfumo wa kati wa sikio umekadiliwa kuwa masaa 25.
Sumu ya ceftriaxone
Kutumia dozi kubw akupita kiasi huongeza hatari ya kufanyika kwa mawe ndani ya njia ya mkojo na kuferi kwa figo.
Dalili za kutumia dozi kubwa kupita kiasi hazijaandikwa lakini hufanana na maudhi ya dawa. Kama dozi ikizidishwa, dawa inaweza kuondolewa haraka kwenye damu kwa kufanyiwa dayalisis.
Maudhi ya ceftriaxone
Kinyesi cheusi kinachonata
Maumivu ya kifua
Kutetemeka
Kikohozi
Homa
Maumvu wakati w akukojoa au ugumu kutoa mkojo
Kuishiwa pumzi
Vidonda kooni
Vidonda au mabaka mekundu kwenye midomo au kinywa
Kuvimba kwa tezi
Kutokwa damu au kuvia damu kirahisi
Uchofu usio kawaida
Maudhi yanayotokea mara chache
Kuharisha
Maudhi yanayotokea kwa nadra sana
Maumivu ya tumbo
Kutokwa damu kwenye fizi
Tumbo kujaa gesi
Kutokw ana damu puani
Kuwa na rangi ya bluu
Kinyesi cheusi
Degedege
Kupumua kwa shida
Kizunguzungu
Mapigo ya moyo kwenda mbio
Maumivu ya kichwa
Kuhisi joto kupanda mwilini
Homa na kutetemeka
Kutokwa na jasho jingi
Kuvimba mwili
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya nyuma ya mgongo
Muwasho
Ongezeko la damu ya hedhi
Ceftriaxone wakati wa ujauzito
Tafiti nyingi hazijafanyika kwa binadamu kuhusu madhara ya dawa hii kwa kijusi tumboni, na zile zilizofanyika kwa wanyama wajawazito zinaonyesha kuwa dawa hii haikusababisha ulemavu kwa kijusi. Hata hivyo matumizi ya dawa hii huweza kuua bakteria rafiki kwenye mwili wa binadamu.
Usugu wa dawa kwenye vimelea
Baadhi ya bakteria wamekuwa hawasikii dawa hii kutokana na kutengeneza usugu kwenye dawa. Unashauriwa usitumie dawa hii pasipo kuandikiwa na daktari wako au kabla ya kufanyiwa vipimo.
13 Juni 2023, 19:18:46
Dawa Ceftriaxone
Imeboreshwa,
12 Februari 2022, 11:42:18
Dawa yoyote ni sumu, usitumie dawa pasipo ushauri wa daktari kuepuka madhara kwenye ogani mbalimbali kama figo na ini. Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari unaweza kusababisha madhara na usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa.
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baad aya kusoma makala hii.
Kupata ushauri zaidi na tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya Mawasiliano yetu au Pata tiba.
Rejea za mada hii:
Bäck SE, et al. Age dependence of renal function: clearance of iohexol and p-amino hippurate in healthy males. Scand J Clin Lab Invest. 1989 Nov;49(7):641–646.
Bax RP, et al. The pharmacokinetics of meropenem in volunteers. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):311–320.
Burman LA, et al. Pharmacokinetics of meropenem and its metabolite ICI 213,689 in healthy subjects with known renal metabolism of imipenem. J Antimicrob Chemother. 1991 Feb;27(2):219–224.
Christensson BA, et al. Pharmacokinetics of meropenem in subjects with various degrees of renal impairment. Antimicrob Agents Chemother. 1992 Jul;36(7):1532–1537.
DAVIES DF, SHOCK NW. Age changes in glomerular filtration rate, effective renal plasma flow, and tubular excretory capacity in adult males. J Clin Invest. 1950 May;29(5):496–507.
Douglas JG, et al. The pharmacokinetics of cefuroxime in the elderly. J Antimicrob Chemother. 1980 Jul;6(4):543–549.
Granerus G, et al. Reference values for 51Cr-EDTA clearance as a measure of glomerular filtration rate. Scand J Clin Lab Invest. 1981 Oct;41(6):611–616.
Harrison MP, et al. The disposition and metabolism of meropenem in laboratory animals and man. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):265–277.
Jones RN, et al. In-vitro studies of meropenem. J Antimicrob Chemother. 1989 Sep;24 (Suppl A):9–29.
Krutzén E, et al. Plasma clearance of a new contrast agent, iohexol: a method for the assessment of glomerular filtration rate. J Lab Clin Med. 1984 Dec;104(6):955–961.
Ljungberg B, et al. Pharmacokinetics of antimicrobial agents in the elderly. Rev Infect Dis. 1987 Mar-Apr;9(2):250–264.