Apium graveolens hufahamika kama celery,ni mmea poli na hutumika sana kama mboga kuliko dawa, matawi yake na mbegu hutumika katika matibabu ya matatizo ya mkojo, baridi yabisi, maumivu ya maungio(athraitiz) .n.k
Arctium lappa asili yake ni Ulaya na Asia, hata hivyo kwa sasa unapandwa sehemu nyingi dunaini katika ukanda wa joto. Hutumika kwenye matibabu ya magonjwa yanayotokana na sumu nyingi kwenye damu kama vile anjaina n magonjwa ya ngozi.
Butyrospermum parkii, hujulikana kwa jina jingine la shea, hufahamika sana Afrika kutokana na uwezo wake wa kutibu magonjwa ya ngozi kavu, pumu ya ngozi na kutumiwa kwenye urembo wa ngozi na nywele kwa wanawake.