top of page

Dawa asilia na matumizi

Cajanus cajan, ni mmea asilia wenye uwezo wa kutibu tatizo la kuharisha, hufahamika kama mbaazi.

Cajanus cajan

Mmea huu umekuwa ukitumika kwenye tiba asilia kama dawa ya kuzuia kuharisha, mmea huu asili yake ni India, na Afrika lakini kwa sasa unapatikana maeneo mengi duniani katika ukanda wa tropiki na hufahamika Kiswahili kama mbaazi.

Cantharanthus roseus, ni ua lenye uwezo wa kutibu saratani ya damu, kisukari na shinikizo la juu la damu

Cantharanthus roseus

Cantharanthus roseus, ni mmea wenye uwezo wa kutibu kisukari, shinikizo la juu la damu na saratani.

Mpapai kwa jina la kisayansi Carica papaya huwa na uwezo wa kutibu manjano, minyoo na malaria

Carica Papaya

Ni mti ambao asili yake ni Amerika ya kati, kwa sasa unalimwa na kustawi vema maeneo mbalimbali Afrika. Matumizi ya mpapai ni mengi na imeandikwa kwenye kumbukumbu kwamba mazao yote ya mpapai yana uwezo kitiba wa kitibu njano, utomvu wake hutibu minyoo, mizizi na majani yake huwa na uwezo wa kupunguza maji mwilini.

Caulophyllum thalictroides dawa asili ya maumivu ya hedhi

Caulophyllum thalictroides

Caulophyllum thalictroides ni mmea poli wenye uwezo wa kutumika kama dawa ya kuimarisha misuli ya kizazi, kupunguza maumivu ya hedhi na kuongeza uchungu . Caulophyllum thalictroides hufahamika kwa jina jingine la ‘blue cohosh’

Chenopodium ambrosioidesni dawa asili ya minyoo

Chenopodium ambrosioides

Mafuta ya Chenopodium ambrosioides yamekuwa yakitumika sana katika nchi nyingi kama dawa asili ya minyoo kwa binadamu. Hii ni kutokana na kuwa na kemikali ya ascaridol ambayo hupooza minyoo na kuwaua.

bottom of page