Combretum glutinosum ni moja ya mmea maarufu katika tiba asili kutokana na uwezo wake wa kupunguza maji mwilini, kushusha shinikizo la juu la damu na kutibu kikohozi. Tafiti nyingi zilizofanyika zimeonyesha matokeo yake mazuri katika tiba.
Ni mmea wenye asili ya Australia hata hivyo hupatikana sehemu nyingi za ukanda wa joto barani Afrika. Huwa na uwezo wa asili kutibu kutibu kikohozi, bronkaitizi, nimonia, UTI, homa, kiungulia, mapigo ya moyo kwenda kasi na dalili za koma hedhi.
Euphorbia hirta ni mmea unaofahamika duniani kote kutokana na uwezo wake mkubwa katika tiba asili haswa kutibu matatizo ya wanawake, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, minyoo, amibiasis na kisonono.
Griffonia simplicifolia ni aina ya mmea unaopatikana Afrika, mbegu zake hutumika kama dawa ya sonona, hofu kuu, kupunguza uzito, maumivu ya kichwa na kukosa usingizi.
Ni mti wa maajabu haswa kwenye matibabu ya ugumba na kukuza matiti kwa mabinti wanaokuwa, hupatikana maeneo mengi afrika hata mbuga za wanyama kama mbuga ya wanyama ya manyara, Tanzania .