Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya allergy ya macho
20 Juni 2021 19:00:32
Dawa ya aleji ya mcho au dawa za mzio, ni dawa zinazotumika kupunguza au kuondoa mwitikio wa macho kwenye viamsha mzio.
Dawa ya mzio/allegy/aleji ya macho
Dawa hizi si kwamba zinatibu kisababishi, bali hupunguza au kuzuia mwitikio wa mwili wako kwenye mzio, ni vema ukaepusha vitu au mazingira ambayo yanakupa mzio kuliko kutumia dawa hizi kwa muda mrefu.
Orodha ya dawa za mzio wa macho
Dawa za mzio wa macho ni;
Azelastine
Cetirizine
Cromolyn
Dexamethasone
Diphenyhydramine
Emedastine
Fexofenadrine
Hydroxypropylmethylcellulose
Levocabastine
Lodoxamine
Loratadine
Methylprednisolone acetate
Necondromil
Olopatadine
Oxymetazoline
Pemirolast
Prednisolone
Sodium cromoglycate
Triamcinolone Acetatonide
Majina mengine ya dawa za allergy
Majina mengine yanayomaanisha dawa za allergy ya macho na hutumika na watu wengine ni;
Dawa za macho mekundu
Dawa za aleji ya macho
Dawa ya mzio kwenye macho
Wapi unaweza kupata taarifa zingine zaidi kuhusu allergy ya macho?
Kupata taarifa zingine kuhusu allergy au mzio wa macho ingia kwenye makala ya 'mzio wa macho' au 'mzio' au 'aleji ya macho' sehemu nyingine katika tovuti hii ya ulyclinic