Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
Dawa ya chembe ya moyo
1 Juni 2022, 17:54:31

Dawa ya chembe ya moyo katika makala hii imemaanisha dawa za kutuliza maumivu yanayotokea sehemu ya chini ya miishio ya fupa titi.
Chembe ya moyo ni maumivu yanayohisia mbele ya kifua, sehemu ya chini mahari ambapo fupatiti huishia na tumbo huanzia. Mara nyingi maumivu haya hutokana na matatizo katika mfumo wa chakula.
Kuna magonjwa na hali mbalimbali zinazoweza kusababisha maumivu ya chembe ya moyo, miongoni mwayo ni:
Kuvimbiwa
Kiungulia
Kucheua tindikali
Kula kupita kiasi
Kutostahimili laktozi
Kunywa pombe
Mvurugiko wa tumbo au kuu la chakula
Henia ya hiata
Vidonda vya tumbo
Vidonda kwenye duodamu
Magonjwa ya kifuko cha nyongo
Ujauzito
Matumizi ya dawa aina Fulani
Umio la Barrett
Maambukizi kwenye kongosho
Matibabu
Matibabu ya maumivu ya chembe ya moyo hutegemea kisababishi, baadhi ya magonjwa kama wa kucheua tindikali, vidonda kwenye tumbo na duodenamu na na umio la Barrett huhitaji matibabu ya muda mrefu.
Kama kama kisababishi ni matumizi ya dawa aina Fulani, daktari atakushauri kubadilisha dawa na kama ni kutokana na kucheua tindikali, dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali zinaweza kukusaidia.
Wakati gani wa kuonana na daktari?
Mara nyingi maumivu ya chembe ya moyo huwa yanasababishwa na sababu zisizo za kuogopesha. Hata hivyo endapo unapata maumivu makali ya chembe ya moyo unapaswa kuonana na daktari mara moja kwa uchunguzi na tiba.
Onana na daktari mara moja kwa huduma ya haraka endapo unapatwa na dalili zifuatazo:
Kupumua kwa shida
Kumeza kwa shida
Hisia za kugandamizwa kifuani
Kukohoa damu
Kutapika damu
Homa kali
Kichefuchefu, kutapika na kuharisha kwa zaidi ya 24
Uchovu mkali
Ili kusoma matibabu ya kila kisababishi, ingia kwenye dawa za kila kisababishi.