Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya kutibu Vajinosis ya bakteria
18 Juni 2021, 13:04:55
Vaginosis ya bakteria ni ugonjwa wa vajinosis ya bakteria ni hali inayoletwa na ongezeko kubwa la bakteria waishio ndani ya uke hivyo kuwazidi bakteria walinzi ambao pia huishi ndani ya uke
Dawa za kutibu vajinosis ya bakteria
Dawa zinazoweza kutumika kutibu vaginosis ya bakteria ni;
Metronidazole (Flagyl)
Tinidazole (Tindamax)
Clindamycin (Cleocin, Clindesse)
Dalili za vaginosis ya bakteria
Wanawake wengi wenye ugonjwa wa vajinosis ya bakteria huwa hawaonyeshi dalili au ishara yoyote, hata hivyo endapo dalili zitatokea zinajumuisha;
Kutokwa na ute mwembamba, rangi ya kijivu au mweupe kama maziwa
Kutokwa na harufu mbaya ukeni mithiri ya harufu ya samaki haswa baada ya kujamiana
Hisia za kuungua, kuwashwa ukeni au maeneo yanayozunguka tundu la uke kwa nje
Maumivu wakati wa kukojoa( kuungua ukeni wakati wa kukojoa au majimaji yanapopita)
Majina mengine ya dawa ya kutibu vaginosis ya bakteria ni
Dawa za bacteria vaginosis
Dawa ya uchafu wa ute wa rangi ya kijivu ukeni