Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt Adolf S, MD
Dawa ya vibarango kwa watoto
6 Desemba 2024, 19:39:15
Utangulizi
Vibarango ni ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na fangasi, huathiri ngozi ya mwili na kichwa. Kwa upande wa watoto vibarango ni ugonjwa unaojitokeza sana hasa kwa watoto wadogo wa shule.
Dawa za kutibu vibarango kwa watoto ni sawa na zile za watu wazima isipokuwa kwa watoto dozi hutolewa kwa kuzingatia uzito wa mtoto.
Orodha ya dawa za kutibu vibarango kwa watoto
Dawa za kutibu vibarango zipo katika mifumo miwili yaani dawa za kupaka na dawa za kunywa kama ifuatavyo .
Dawa za kupaka
Hutumika kutibu maambukizi madogo na ya wastani, dawa hizo ni ;
Benzoic acid (Whitefield)
Miconazole
Clotrimazole
Terbinafine
Ketaconazole
Dawa za kunywa
Hutumika kutibu maambukizi makubwa na maambukizi sugu yanayojirudia rudia, dawa hizo ni;
Griseofulvin
Terbinafine
Ketakonazole
Fluconazole
Tahadhari kwa msomaji
Makala hii imeandikwa kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii.
Usitumie maelezo katika makala hii kufanya matibabu au usitumie dawa zilizoelezwa bila kuandikiwa na daktari.