Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
Dawa za fangasi wa miguuni
10 Julai 2023, 11:31:43
Maambukizi haya ya Tinea pedis yanaathiri maeneo ya kanyagio na katikati ya vidole vya miguu, ni maambukizi yaliyoathiri binadamu kwa kipindi kirefu kabla ya kugunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1908. Fangasi anayesababisha maambukizi haya hufahamika kama Trichophyton rubrum wanaopatikana sana maeneo ya mashariki mwa bala la Ulaya na sehemu za Afrika na bala la Australia. Matumizi ya viatu vya kufunika, vita, kuongezeka kwa njia za kusafiri, kutembea kwenye makundi kumeonekana kuongeza wingi wa ugonjwa huu.
​
Dawa Za Kutibu Fangasi Wa kanyagio na maeneo katikati ya vidole vya miguu- Tinea pedis
​Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu ni pamoja na;
​
Dawa ya kupaka ya clotrimazole
Dawa ya kupaka ya Econazole
Dawa ya kupaka ya Ketoconazole
Dawa ya kupaka ya Miconazole
Dawa ya kupaka ya Oxiconazole 1%
Dawa ya kupaka ya Sertaconazole
Luliconazole
Ciclopirox
Naftifine
Terbinafine
Butenafine
Itraconazole
Fluconazole
Dawa ya kupaka ya Aluminum lactate
Dawa ya kupaka ya Urea