Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
Dawa za kichefuchefu na kutapika
11 Julai 2023, 08:15:57
Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia kichefuchefu na kutapika kusababishwa na matatizo mbalimbali ndani ya mwili yanayoweza kuwa ya hatari au yasiyo ya hatari. Endapo mtu ana kichefuchefu na kutapika, kitiba huashiria kuna shida fulani inaendelea ndani ya mwili inayosababisha dalili hizi (mfano maambukizi ndani ya mfumo wa chakula-minyoo, amoeba, kipindupindu,homa ya matumbo-typhoid, maambukizi kwenye mfumo wa fahamu n.k)
Kupata ushauri wa daktari ni lazima kabla ya kutumia dawa yoyote ya kuzuia kichefuchefu na kutapika. Wakati mwingine kutapika ni bora kuliko kuzuia kutapika kwa sababu huondoa tatizo ndani ya mwili,mfano mtu amekunywa sumu au ana maambukizi ndani ya tumbo ambapo mwilikwa asili yake unataka kuyatoa nje ya tumbo kwa njia ya kutapika. Lakini pia kutapika kupita kiasi kunaweza kusababisha mtu kuishiwa nguvu na kulegea, figo kuferi ghafla, mapigo ya moyo kutokueleweka na hata kifo hii ni kwa sababu kupoteza madini muhimu na maji mwilini.
Orodha ya dawa
Dawa zinazoweza kuzuia kutapika ni pamoja na;
Promethazine (phenergan)
Prochlorperazine(compazine)
Metoclopramide(reglan)
Diphenhydramine
Dawa zilizoorodheshwa hapa chini huzuia kupata kichefuchefu na kutapika;
Ondasetron
Promethazine
Prochlorperazine
Prochlorperazine
Cyproheptadine
Diphenhydramine
Amitriptyline
Propanol
Phenobarbital
Topiramate
Zonisamide
Erythromycin
Sumatriptan
Lorazepam