Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kuchelewesha hedhi
15 Juni 2021 14:44:00
Dawa za kuchelewesha hedhi au mens ni dawa zinazozuia hedhi kutokea.
Dawa za kucheewesha hedhi ni nini?
Dawa za kuchelewesha hedhi au mens ni dawa zinazozuia hedhi kutokea. Dawa hizi hufanya kazi kwa kuzuia ukuta wa hedhi kuvunjika, dawa hizi huwa na homon ya progesterone. Dawa hizi mara nyingi huanza kutumia siku 2 hadi 4 kabla ya kuanza kwa hedhi
Orodha ya dawa za kuchelewwesha hedhi ni;
Norethisterone (norethisterone), Primolut N
Medroxyprogesterone acetate
Dawa za uzazi wa mpango zenye mchanganyiko wa progesterone na estrogen kama;
Azurette
Beyaz
Enpresse
Estrostep Fe
Kariva
Levora
Loestrin
Natazia
Dozi unayotakiwa tumia ili kuchelewesha hedhi ni ipi?
Kufahamu dozi na endapo inafaa kwako kutumia dawa hizi, wasiliana na daktari wako
Kumbuka
Utakaposimama kutumia dawa hizi, hedhi inategemea kuanza ndani ya siku 2 hadi 3
Namna gani ya kutumia dawa za uzazi wa mpango zenye mchanganyiko wa estrogen na progesterone kuchelewesha hedhi?
Kuchelewesha hedhi kwa kutumia dawa za uzazi wa mpango, unatakiwa kwanza uwe mtumiaji wa dawa hizo kila siku. Utakapokaribia kwenye vidonge vyenye rangi tofauti za vingine, anza kutumia pakiti nyingine kuendelea na vidonge vyenye rangi ambayo ulikuwa unatumia na kuachana na vile vyenye rangi tofauti kwa muda ambao utataka hedhi yako kusimama. Endapo unataka kurejesha hedhi, acha vidonge hivyo na tumia vidonge vyenye rangi nyingine ambayo ulikuwa hujavitumia kwa muda wa siku saba. Kisha anza kutumia vidonge vyako kama ulivyopangiwa na daktari baada ya hedhi kusimama.