Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD.
Dawa za kukausha vidonda ukeni
17 Desemba 2024, 16:25:15
Utangulizi
Vidonda ukeni hasa kwenye mashavu inaweza kuwa dalili ya maambukizi au maradhi mengine kama vile magonjwa ya ngozi yasiyosababishwa na maambukizi.
Magonjwa ya zinaa yanachangia asilimia nyingi ya vidonda ukeni, hivyo katika makala hii dawa zilizoanishwa ni zile zinazotumika kutibu vidonda vinavyosababishwa na magonjwa ya zinaa mfano kaswende, pangusa, herpazi n.k.
Orodha ya dawa za kutibu vidonda ukeni
Dawa zinazotumika mara kwa mara kutibu au kukausha vidonda ukeni ni kama ifuatavyo;
Benzyl Penicillin (Pen G)
Azithromycin
Erythromycin
Ciprofloxacin
Doxycycline
Acyclovir
Valacyclovir
Famciclovir
Ceftriaxone
Daktari anaweza kukuandikia dawa ya kundi moja au zaidi kutokana na kisabaishi. Unapaswa kuwasiliana na daktari ili kufahamu dawa gani inakufaa wewe kulingana na kisababishi.
Tahadhari kwa msomaji
Makala hii imeandikwa kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii, hivyo usitumie maelekezo yake kufanya matibabu yako.