Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Salome A, MD
Dawa za Kuongeza uchavushaji wa mayai
10 Julai 2023, 11:40:15
Zipo dawa ina mbalimbali za kuongeza uchavushaji wa mayai kwa mwanamke na kumfanya apate mimba kwa haraka na wakati mwingine kusababisha mimba ya Watoto Zaidi ya mmoja. Sehemu hii imezungumzia kuhusu dawa jamii ya Choriogonatrophin alpha.
​
Dawa hizi nyingi zipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Gonadotrophin, yapo majina ya aina tofauti ya dawa hizo kutokana na kiwanda kinachozalisha lakini kazi yake ni moja.
Â
Namna ya dawa zinavyofanya kazi
Dawa jamii hii huongeza uzalishaji wa homoni ya Folicle stimulating Homoni (FSH) .Kazi ya FSH ni kuamsha uchavushaji wa yai kutoka kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai kwa mwanamke(ovari), dawa hii hufanya kazi kwa wanawake wale tu ambao ovari zao hazina matatizo ya awali bali kutokana na Matatizo mengine mwilini basi mayai yanashindwa kuzalishwa.
​
Dawa hizi zikitumiwa na wanaume huweza kuongeza uzalishaji wa mbegu kiume(manii) na pia ufanyaji kazi wake huwanza kuanzia mienzi mitatu hadi 18. Dawa hizi hutumika kwa kuchomwa sindano chini ya ngozi ya tumbo
Â
Matumizi
Kuamsha uzalishaji wa mayai kwa mwanamke.
Kuamsha uzalishaji wa manii(mbegu za kiume)
Â
Maudhi ya dawa yanayoweza kutokea ni pamoja na;
Asilimia 1 hadi 10 ya watu wanaotumia dawa hupata
Kupata vifuko vya maji kwenye kiwanda cha mayai
Kuamsha kwa kasi uzalishaji wa mayai kwenye kiwanda cha mayai
Maumivu ya tumbo
Kutapika
Miunguzo sehemu ya kuchomea sindano
​
Watu chini ya asilimia 1 hupata
Maumivu ya titi
Jeraha kwenye shingo ya kizazi
Kukojoa protini ya albumin kwenye damu
Maumivu ya mgongo
Mapigo ya moyo kutokwenda sawa
Kizunguzungu
Kubadilika kwa hali ya mtu
Virusi vya herpes kwenye sehemu za siri
Kupanda kwa sukari kwenye damu
Kuwashwa
Maambukizi ya UTI
Kutokwa na damu ukeni
Michomo asilia kwenye uke
​
Dalili zngine ambazo haifahamiki ni watu kiasi gani wanapata huwa pamoja na
Maumivu ya kichwa
Kuwa mkali
Msongo wa mawazo
Mwili kuvia maji
Kuwa mchovu
Matiti kukua kwa wanaume
Ujana mzuri
Mwili kuchoka sana
Kuganda kwa damu kwenye mishipa ya artery
Kupasuka kwa vifuko vya maji vya ovary
Â
Mfano wa dawa huwa pamoja naÂ
Urofollitrophin
chorigonatrophin alpha
fertinorm HP
Gona-f
MenopurÂ
Menotropins
Novareal
Ovidrel
Pregny
Repronex
​
Dawa zingine
Dawa zingine ni jamii ya Selective  Estrogen receptor modulator ambazo ni;
Bazedoxifene/conjugated estrogens,Â
Clomid, clomiphene,
Duavee
Evista
Ospemifene
Osphena
Raloxifene
Serophene
Tamoxifen
Majina mengine
Dawa za kuongeza uzalishaji wa mayai hujulikana pia kama
Dawa za kutibu ugumba kwa wanawake
Dawa za kutibu ugumba kwa wanaume
Dawa za kuongeza uzalishaji manii