top of page
Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, M.D
Dawa za kutibu Tinea Versicolor
10 Julai 2023, 17:29:48
Dawa za kutibu fangasi wa kiwiliwili hufahamika kama dawa za kutibu fangasi wa kifuani na maeneo ya mgongoni pia huitwa Tinea Versicolor
​
Maambukizi ya Tinea Versicolor ni maambukizi ya fangasi yanayofahamika sana, huwa na sifa ya kuwa na duara ndogo au kubwa mwilini yenye mwonekano wa rangi iliyokolea au iliyopauka kuliko sehemu nyingine maeneo ya kifuani na juu ya mgongo. Fangasi wanaosababisha ugonjwa huu ni Malassezia Globosa, Malassezia sympodialis na Malassezia furfur. Fangasi hawa wanaweza kuonekana kwenye Ngozi isiyougua na Ngozi inayougua.
​
Orodha ya dawa za fangasi wa kiwiliwili
Dawa zinazotumika kutibu tatizo hili ni pamoja na;
Terbinafine
Clotrimazle
Ketoconazole
Ciclopirox
Butenafine
Naftifine
Econazole
Oxiconazole
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Julai 2023, 17:53:39
BNF 2019
bottom of page