Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za kutoa mimba
8 Juni 2021 14:27:55
Kutoa mimba ni kitendo cha kukatisha maisha ya kijusi aliyepo tumboni, hii inaweza kufanyika kwa kutumia dawa au kutumia njia ya upasuaji mdogo au kusafisha kizazi. Kutoa mimba kwa nchi nyingi ni kinyume na sheria, hata hivyo baadhi ya nchi pia zinaruhusu kitendo hichi kufanyika. Mama anaweza pata madhara endapo atatumia dawa bila msaada wa daktari au mtaalamu wa afya ambaye amebobea kwenye kazi hiyo.
Dawa zilizoorodheshwa hapa chini zina uwezo wa kutoa mimba ndogo au kubwa, wasiliana na daktari wako kuhusu namna ya kutumia, aina, dozi na umri gani dawa zilizoorodheshwa hapa chini zinaweza kufanya mimba itoke.
Dawa zenye uwezo wa kutoa mimba
Mifepristone (Mifeprex)
Misoprostol (Cytotec)
Methotrexate (Otrexup, Rasuvo)
Carboprost Tromethamine
Prostine E2 ( dinoprostin)
Oxytocine (Pitocin)
Kuna dawa zingine hutumika na dawa za kutoa ujauzito?
Ndio kuna dawa zingine hutumika baada ya kutumia dawa za kutoa mimba ili kuzuia, maumivu au maambukizi kwenye kizazi. Kumbuka unapotoa mimba, shingo ya kizazi hufunguka kwa muda mrefu hivyo huweza kuruhusu maambukizi kuingia.
Dawa za maumivu
Paracetamol
Dawa za antibayotiki
Inaweza kutumika mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja.
Metronidazole
Ampiciclox (Ampicilin na cloxacillin)
Doxycycline
Azithromycin
Gentamicin
Clindamycine
Levofloxacin
Imipenem
Piperacillin‐tazobactam
Ticarcillin‐clavulanate
Dawa za kusinyaza kizazi baada ya mimba kutoka
Methergine
Ergotamine
Madhara ya kutoa mimba kwa dawa
Madhara yanayoweza kutokea kutokana na kutoa mimba kwa kutumia dawa huwa katika makundi mawili kama yaliyoelezewa hapo chini yaani;
Madhara ya muda mfupi
Madhara ya baadae
Madhara ya muda mfupi ya kutoa mimba
Kuishiwa damu
Kupata maambukizi kwenye kizazi
Kubadilika kwa hedhi
Kuoza kizazi
Kifo
Madhara ya baadaye ya kutoa mimba kwa dawa
Kubadilika kwa hedhi
Ugumba