Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za maumivu ya chembe ya moyo
7 Juni 2021 13:20:35
Chembe ya moyo au kwa watu wengine hufahamu kama maumivu ya chemba ya moyo katika Makala hii imetumika kumaanisha maumivu ya eneo la juu(epigastriki) ya tumbo yanayoweza kusababishwa na matatizo mbalimbali, na hufahamika kwa jina jingine kama kiungulia. Maumivu haya hutokea kwenye makutano ya mfupa wa sternum wa na misuli ya tumbo inapoanzia (angalia picha) kisha huuweza sambaa kuelekea juu katikati ya kifua kwenye mfupa wa ziwa (sternum).
Je kuna dawa moja ya kutibu chemba ya moyo (kiungulia)?
Hapana. Dawa zinazotumika kutibu maumivu ya chembe ya moyo hutegemea kisababishi.
Je ni nini husababisha chembe ya moyo
Baadhi ya visababishi vinavyochangia kwa asilimia kubwa kusababisha maumivu ya chemba ya moyo au kiungulia ni;
Kucheua tindikali
Kula chakula kingi (kula kupita kisai)
Kutostahimili laktosi
Pombe
Kuvimbiwa
Henia ya Hiatal
Michomo kwenye umio
Michomo tumboni
Vidonda vya tumbo kutokana na maambukizi ya H.pylori
Vidonda vya tumbo kutokana na uzalishaji wa tindikali
Umio la Barrett’s
Mawe ndani ya kibofu cha nyongo
Ujauzito
Unapata wapi dawa za matatizo zilizoorodheshwa hapo juu?
Ili kusoma zaidi kuhusu dawa za maumivu ya chembe ya moyo, chagua kisababishi mfano 'dawa ya kuvimbiwa' kisha tafuta kwenye bokski juu ya tovuti hii iliyoandikwa 'Tafuta chochote hapa...'
Mambo mengine unayotakiwa kufahamu
Ili kufahamu ni nini kinasababisha maumivu ya chemba ya moyo au kiungulia, unapaswa kufahamu dalili zingine au kusoma magonjwa ambayo yanasababisha maumivu ya chemba ya moyo ambayo tayari yameshaorodheshwa hapa juu.
Tuambie ni nini unataka kufahamu zaidi
Endapo unaswali au ushauri wasilisha kupitia mawasiliano yaliyo chini ya tovuti hii.