Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, M.D
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Dawa za maumivu ya majeraha
11 Julai 2023, 10:23:29
Dawa hizi zinaweza kupatikana kama kidonge, mafuta au maji maji. Hivyo huweza kutumika kwa njia ya kumeza, kuchoma sindano au kupaka sehemu iliyoathirika.
Endapo maumivu yapo sehemu moja ya mwili ili kuzuia madhara na endapo unatumia muda mrefu Zaidi ya siku 3 inashauriwa kutumia dawa ya kupata ambayo uwepo wake kwenye damu unakuwa mdogo sana kiasi cha kutoleta madhara.
Wasiliana na dakitari wako siku zote kabla ya kutumia dawa za maumivu maana zina mashara mwilini endao zitatumika bila ushauri kwa kusababisha matatizo kama, kuferi kwa ini, figo, kuyeyuka na kutokwa na damu kwenye maeneo ya mwili yaliyo wazi mfano pua, mdomo na maeneo yenye majeraha.
Paracetamol
Diclofenac
Ibuprofen
Aspirin
Kumbuka Aspirin hautakiwi kutumika kwa watoto wadogo chini ya miaka miwili kwa sababu ya madhara yake.