top of page
Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, M.D

Dawa za Tinea Nigra

10 Julai 2023, 18:41:02
Image-empty-state.png

Maambukizi ya fungasi kwenye viganja vya mikono na miguu kwa jina jingine hufahamika kama Tinea Nigra husababishwa na fungasi mwenye jina la Hortaea werneckii  au Stenella araguata. Maambukizi haya hutokea maeneo ya viganja vya mikono na miguu au sehemu nyingine za mwili kama maeneo ya katikati ya vidole.


​Orodha ya dawa

Dawa zinazoweza kutibu maambukizi haya ni;

  • Clotrimazole

  • Ketoconazole

  • Miconazole

  • Ciclopirox

  • Terbinafine

  • Endecyclenic acid

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Julai 2023, 18:51:57
BNF 2019
bottom of page