top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

​

Dawa za kutibu maambukizi ya virusi vya herpes

​

Virusi vya herpes husababisha maambukizi ya herpes na varisela zoster(mkanda wa jeshi). Ugonjwa wa herpes unaotokea kwenye macho na midomo maeneo mengine ya ngozi husababishwa na kirusi cha herpes aina ya 1, maambukizi kwenye maeneo ya uke husababishwa na kirusi cha herpes aina ya 2.

​

Matibabu ya maambukizi ya kirusi huyu hutakiwa kuanza mapema iwezekanavyo haswa ndani ya siku tano toka maambukizi yameonekana. Kwa watu wenye kinga za mwili zilizo imara, matibabu ya maambukizi kwenye mashavu ya uke, midomo na macho huweza hufaa sana dawa za kupaka. Maambukizi makali, kwa watoto au maambukizi kwa watu wenye kinga za mwili zilizochini, dawa za kuingia mwilini kwanjia ya mishioa hufaa zaidi. Maambukizi ya kujirudia katika maeneo ya siri hutibiwa kwa dawa za kunywa. Kujirudia kwa ugonjwa kwa watu wenye kinga za mwili zilizo chini huashiria virusi vimekuwa sugu dhidi ya dawa.

​

Maambukizi ya varicella zoster(mkanda wa jeshi)

​

Bila kujali wingi wa kinga za mwili, watoto wachanga wenye tetekuwanga wanatakiwa kutibiwa kwa dawa za mishipa ili kupunguza kupata ugonjwa mkali. Dawa za kunywa kwa watoto wadogo hazishauriwi. Watoto wadogo wenye tetekuwanga na wapo kati ya umri wa mwaka mmoja na miaka 12 hupata dalili zisizo kali,hivyo matumizi ya dawa huwa hayashauriwi.

​

Dawa zinazotumika ni pamoja na;

​

  • Inosine pranobex

  • Acyclovir

  • Famciclovir

  • Valaciclovir

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako au mtaalamu wa afya kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale yanayodhuru afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa ushauri zaidi na Tiba kupitia namba za simu au kubonyeza pata tiba chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa mara ya mwisho 27.05.2020

​

Rejea zamada hii

​​

  1. BNF 76. toleo la septemba-march 2018-2019

bottom of page