Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
Dawa za kutibu maumivu kwa wagonjwa wa kisukari- Diabetic Neuropathy
​
Kwa matibabu ya maumivu yanayotokana na kuharibiwa kwa mfumo wa fahamu kwa sababu ya kisukari, mgonjwa anaweza kutumia dawa za kawaida za kuondoa maumivu. Kwa maumivu makali na sugu dawa aina zingine zinatakiwa kutumika. Kwa baadhi ya wakati dawa za kulegeza misuri huweza kuwa na faida kwa mgonjwa wiki mbili za kwanza za kuanza matibabu ya maumivu.
​
Kila baada ya wiki 6 mgonjwa anapaswa kuchunguzwa ili kuona kama kuna uhaja wa kupunguza dozi au kuacha kabisa matumizi ya dawa za maumivu endapomaumivu yanaisha. Dawa zinaweza kuanzishwa upya endapo dalili ya maumivu imeanza upya. Madawa yafuatayo yanatumika, ingawa kwa baadhi ya nchi baadhi ya dawa hazijaruhusiwa kutumika na shirika la dawa la nchi husika;
​
-
Ibuprofen
-
Naproxen
-
Capsaicin
-
Gabapentin (Neurontin)
-
Carbamazepine
-
Phenytoin
-
Amitriptyline
-
Imipramine
-
Nortriptyline
-
Duloxetine
-
Citalopram
-
Paroxetine
-
Erythromycin
-
Polyethylene glycol
-
Bethanechol Hydrochloride
-
Fludrocortisone
-
Desipramine
-
Metoclopramide
​
​
Imeboreshwa 12.02.2020