Mwandishi:
Dkt. Peter A, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa za U.T.I
31 Mei 2022, 14:37:12
UTI kwa asilimia zaidi ya 80 husababishwa na maambukizi ya bakteria ingawa kwa baadhi ya wagonjwa haswa wale wenye UKIMWI, kisukari, wenye matatizo ya maumbile ya mfumo wa mkojo na wanaotumia dawa za kushusha kinga za mwili huweza kupata U.T.I inayotokana na maambukizi ya fangasi, virusi na protozoa.
Mgonjwa wa UTI anaweza kuwa na UTI iliyosababishwa na bakteria aina moja au zaidi ya moja. Maambukizi hayo hutibiwa kwa kutumia dawa za kuua bakeria husika zenye jina la antibayotiki.Â
Dawa zilizooroswshwa hapa chini zinatibu maambukizi ya UTI kutokana na bakteria. Dawa nyingi za kutibu UTI isiyo sugu.Â
Uchaguzi wa dawa za kutibu U.T.I hutegemea mambo malimbali kama vile, aina ya bakteria, fangasi au kirusi aliyesababisha, hali ya mgonjwa, aina ya UTI na hali ya mwitikio wa kimelea kwenye dawa.
Orodha ya dawa za kutibu UTI
Ifuatayo ni orodha ya dawa za kutibu UTI. Kusoma zaidi bofya dawa husika
Ciprofloxacin
Gentamycin
​UTI isiyo kali
UTI isiyo kali kwa wanawake dawa zinazotumika ni;
​
Maamuzi ya kutumia dawa aina fulani
Unaamuaje kuchagua kutumia dawa aina fulani kwa ajili ya kutibu UTI?
Uchaguzi wa dawa ya kutibu UTI hutegemea mambo yafuatayo;
​
Dawa inayofanya kazi kwenye eneo unaloishi- kuna baadhi ya dawa zinofahamika kutibu UTI na kwa sasa hazitibu kutokana na bakteria wanaosababisha UTI kutosikia dawa hizo(kuwa sugu) hivyo dawa itayochaguliwa kutumia ni ile tu ambayo inaweza kuua bakteria wanaosababisha UTI.
Dawa aina ya amoxclav,cefdinir, cefaclor, cefpodoxime-proxetil zinaweza kutumia endapo dawa zinazotakiwa kutumika hapaswi kutumia kulingana na hali ya mgonjwa.
Dawa Fosfomycin na nitrofurantoin inatakiwa kuepukwa kutumika kwa mgonjwa mwenye maambukizi ya awali ya UTI iliyo kwenye mfumo wa juu wa mkojo(figo)
Dawa aina ya (TMP-SMX)inaweza kuzuiwa kutumika ili kuandoa usugu wa bakteria kwenye dawa
Dawa jamii ya fluoroquinolones zitumike kwa UTI sugu tu
Majina mengine
Makala hii imejibu maswali kuhusu;
Dawa nzuri ya U.T.I
Dawa za kutibu UTI
Dawa za kutibu U.T.I sugu