Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, M.D
Mhariri:
Dkt. Salome A, M.D
Dawa za maumivu ya kichwa
11 Julai 2023, 09:43:45
Maumivu ya kichwa yanaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali, matatizo hayo yanaweza kuwa ya hatari au yasiyo ya hatari, mfano maumivu ya kichwa yanayosababishwa na ugonjwa wa maambukizi kwenye mfumo wa fahamu huweza kuleta madhara makubwa na kifo endapo hayajatibiwa haraka kwa kutumia dawa zinazotibu tatizo hilohata kama ukitumia dawa za kutuliza maumivu ya kichwa. Matatizo mengine ya maumivu ya kichwa mfano, kulala vibaya, kujigonga kichwani, msongo wa mawazo, kipanda uso n.k huweza kutulizwa na dawa za maumivu pasipo kuhofu wakati unasubiria kwenda kupata uchunguzi na tiba Zaidi kutoka kwa daktari wako.
​
Orodha ya dawa
Dawa unazoweza kutumia kwa ajili ya kutuliza maumivu ya kichwa ni pamoja na;
Naproxen
Ketoprofen
Ketorolac
Indomethacin
Asprin
Barbiturates
Ergotamine tartrate
Dihydroergotamine
​
Dawa mchanganyiko
Dawa za mchanganyiko ni kama;
​
Fiorinal(butalbital, aspirin na caffeine)
Acetaminophen-(tyenol, panadol na aspirin)
Tylenol-Acetaminophen na codein
Percocet(acetaminophen na oxycodein)