Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020 17:34:25
Amoxyclav
Amoxyclav ni dawa ya antibayotiki yenye mchanganyiko wa Amoxicillin na Clavunic acid, dawa hi hujulikana kwa jina jingine la amoxiclav, aphaclav. Hutumika kutibu maambukizi mbalimbali ya Bakteria kwa binadamu Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia ukuaji na utengenezaji ukuta wa nje wa bakteria hivyo kuzuia kuzaliwa kwa bakteria wapya. Amoxclav imekuwa ikitumika kama dawa nzuri ya kutibu maambukizi kwenye njia ya hewa, sikio la kati, sainas, ngozi na njia ya mkojo.
Fomu ya na uzito wa dawa Amoxyclav
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na kimiminika Kutokana na kupatika kwenye fomu ya kidonge na kimiminika huweza kutumiwa na Watoto pamoja na watu wazima. Amoxclavu huwa na mchanganyiko wa miligramu 500 amoxicillin na miligramu 125 za clavulanic acid Vidonge vya kunywa huwa na uzito mbalimbali kwa kila miligramu 125 za clavulanic asidi mfano
228.5/125
250/125
500/125
875/125 Dawa ya kunywa huwa na uzito mbalimbali wa kiini cha dawa cha amoxcillin na clavulanic aside.
Unaweza tumia Amoxyclav na chakula?
Amoxyclav hufyonzwa vizuri inapotumika pamoja na chakula, hivyo Unashauri kutumika pamoja na chakula jinsi utakavyoshauriwa na daktari wako.
Maudhi ya Amoxyclav
Mzio
Homa
Kuhara
Maumivu ya maungio ya mwili
Manjano
Kutokwa na damu kirahisi au kuumia kirahisi
Kutokwa na damu nyingi wkati wa hedhi
Kubadilika rangi kwa meno
Kichefuchefu na kutapika
Kubadilika radha ya chakula
Degedege
Maumivu wakati wa kujamiana
Kuvimba uso, lipsi, kope, ulimi, mikono na miguu
Choo kuwa cheusi kama rami
Maumivu ya misuli na jointi
Kusinzia sinzia
Mapigo ya moyo kwenda vibaya
Amoxyclav hutibu nini?
Amoxyclav hutumika kutibu maambukizi ya bakteria kwenye;
Mfumo wa kati wa sikio
Pua au sinusaitis
Mfumo wa chini juu wa upumuaji
Ngozi
Tonses na falinksi
Mfumo wa chini wa upumuaji
Tumbo ( Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H. pyroli)
Nutropenia iliyosababishw ana homa homa
Mfumo wa mkojo
Magonjwa yanayotibiwa na amoxyclav
Amoxyclav huwa na uwezo wa kutibu magonjwa yaliyosababishwa na bakteria kama;
Otaitis ya mfumo wa kati wa sikio
Sinusaitis
Nimoni
Jipu kwenye ngozi
Tonses na falinjaitis
Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H. pyroli
Nutropenia iliyosababishwa na homa homa
UTI
Dawa zenye mwingiliano na Amoxyclav
Amoxiclav huwa na mwingiliano na dawa zifuatazo:
Chanjo ya BCG kwa watoto
Doxycycline
Tetracycline
Methotrexate
Chloramphenicol
Clarithromycin
Warfarin
Vitamin K
Allopurinol
Anticoagulants
Dawa za uzazi wa mpango
Methotrexate
Probenecid
Dawa zisizopaswa kutumika na amoxyclav
Usitumie dawa hizi kwani huwa namwingiliano mkali wa amoxyclav
Pexidartinib
Pretomanid
Wakati wa kuchukua tahadhari kwa mtumiaji wa amoxyclav
Wagonjwa wenye mzio na dawa kundi la cephalosporins au carbapenems
Wagonjwa wenye utendaji kazi wa figo <30 mL/dakika
Hatari ya maambukizi makali ya bakteria mbalimbali
Kuota harara wakati wamatumizi
Wagongwa wasiopaswa kutumia Amoxyclav
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na Penicillin
Wagonjwa wenye shida ya ini ambao ishawahi sababishwa na Amoxcillin au Clavunic acid
Amoxyclav itumike kwa tahadhari kwa wagonjwa wapi?
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao:
Wenye aleji na Cephalosporins
Historia ya kuwa na manjano ya kukaa kutokana na matumizi ya amoxiclav
Kama akiharisha zaidi ya Amoxcillin ikitumika yenyewe
Wagonjwa wenye shida ya ini
Dawa hii haipaswi kutumika kwa watu ambao hawana Maambukizi ya bakteria ili kuepusha dawa kuishiwa nguvu na vimelea kuwa sugu.
Matumizi ya Amoxyclav Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Amoxyclavu haipaswi kutumika kwa mama mjamzito isipokuwa endapo faida za matumizi zinazidi madhara yanayoweza kujitokeza. Fuata maelekezo ya daktarin wako kabla ya kutumia dawa hii. Soma kuhusu matumizi ya amoxyclav kwa mama mjamzito na anayenyonyesha kwenye mada za 'Ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha' ndani ya tovuti hii.
Je amoxyclav inatumika kwa mama anyenyonyesha?
Soma kuhusu matumizi ya amoxyclav kwa mama mjamzito na anayenyonyesha kwenye mada za 'Ushauri wa dawa kipindi cha ujauzito na kunyonyesha' ndani ya tovuti hii.
Je endapo utasahau dozi yako ya Amoxyclav ufanyaje ?
Endapo umesahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka dozi uliyosahau na kuendelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:49:21
Rejea za mada hii:-