Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
6 Aprili 2020 10:25:40
Atazanavir
Atazanavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI (ART) na ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaz inhibita- PIs
PIs hutumika kuzuia Kimeng’enya cha proteaz ambacho husaidia kirusi cha HIV kukomaa, kwa kuzuia kirusi cha HIV kukomaa inafanya virusi vya UKIMWI visiendelee kushambulia seli za CD4. Kinga ya mwili huimarika kwa sababu haishambuliwi Zaidi na VVU
Fomu na rangi ya Atazanavir
Dawa hii hupatikana katika fomu ya unga au tembe. Tembe inaweza kuwa na uzito wa miligramu, 100, 150, 200 na 300
Rangi yake ni huweza kutofautiana kutokana na kampuni iliyozalisha dawa.
Dawa hii hutumika ikiwa imeunganika na dawa zingine kupambana na maambukizi ya VVU aina ya HIV-1
Atazanavir inaweza kutumika na chakula?
Dawa huweza kutumika pamoja na chakula
Dawa zilizokundi moja na Atazanavir
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Atazanavir (ATV) ni zifuatazo :
Lopinavir (lpv)
Ritonavir
Darunavir(drv)
Atazanavir
Indinavir
Ritonavir
Nelfinavir
Aptivus
Crixivan
Fosamprenavir
Invirase
Kaletra
Lexiva
Norvir
Prezista
Reyataz
Saquinavir
Tipranavir
Viracept
Kazi ya Atazanavir
Kazi za Atazanavir (ATZ) ni kama zifuatazo:
Huunganishwa na dawa zingine za kuthibiti VVU kwa ajili ya matibabu ya VVU. Baadhi ya muunganiko wa dawa ni pamoja na; Lamivudine (3TC) +Atazanavir (ATV)
Dawa itumike kulingana na maelekezo ya daktari wako
Dawa zisizopaswa kutumika kwa pamoja na Atazanavir
Atazanavir haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Alfozosin
Cabergoline
Carbamezapin
Corbimetinib
Ergotamine
Erythromycin
Rifampin
Pimozide
Tahadhari kwa watumiaji wa Atazanavir
Haipaswi kuchanganywa na Proten Pump Inhibitors
Inapaswa kukatishwa endapo vipele na aleji vitatokea
Mgonjwa anayetumia dawa hii huweza kuwa na sukari ya juu
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Atazanavir
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Mgonjwa mwenye aleji nayo
Mgonjwa mwenye shida ya ini
Matumizi ya Atazanavir kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii haina madhara kwa mama mjamzito na mtoto lakini huwa na maudhi madogo madogo
Matumizi ya Atazanavir kwa mama anayenyonyesha
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote japo dawa hii haina madhara kwake mtoto licha ya kuwa huwa inapita kwenye maziwa
Maudhi ya Atazanavir
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:
Kuwa na homa
Kukohoa
Maumivu kwenye misuli
Kuharisha
Kichwa kuuma
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Tumbo kuuma
Likamu mwilini kuongezeka
Je endapo utasahau dozi yako ya Atazanavir ufanyaje?
Dawa hii hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV endapo utasahau dozi yako, tumia muda uliokumbuka na Kuendelea na muda huo siku inayofuata kama ulivyoelekezwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:49:40
Rejea za mada hii:-